1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Kama watanzania Wanawachagua wabunge wa aina ya wale waliopo unategemea Rais afanyeje zaidi ya kuhakikisha anatekeleza matakwa ya wengi ambao walimpelekea wabunge wa aina hiyo na wakampata Spika wa aina hiyo.Wewe unadhani tunalo Bunge la kupinga matakwa yake Rais anayotaka yapite?
Hebu kuwa mkweli, kwa Spika wa "design" ya Ndugai,ndiyo wa kupinga sheria atakayoileta Rais na atakayotaka ipite?
Yeye ataanza kuvurugana na Bunge la wananchi?
Hebu tusiwe wanasiasa Uchwara na wasio na maarifa kama Mbowe anayeua upinzani kwa umaarufu na maslahi binafsi kwa kung'ang'ania Uenyekiti.
Tuwaambie ukweli watanzania kuwa Kosa ni la kwao sio Serikali. Serikali inatekeleza kile kilichopangwa Karne nyingi zilizopita.
Miaka mingi haya tunayoyaona yalishapangwa kinachofanyika ni utekelezaji tu. Serikali imejitahidi sana kutekeleza.
Bunge kazi yake ni kuhakikisha serikali inatekeleza majukumu yake ipasavyo. Sasa kama serikali inatekeleza majukumu yake basi Bunge sio lazima liiwajibishe kila Mara.
Hayo mengine ya kuwa na wabunge wa binafsi na wanaojipendekeza ni la kuwaachia wapiga kura.
Tunaona hata wapinzani hakuna wabunge Huru zaidi ya kujipendekeza tu kwa wenyeviti wao na wengine kujipendekeza kwa CCM ili wanunuliwe na kurudishwa Bungeni kwa msaada wa bunduki na mabomu ya dola. Sasa watu kama hao hatuwezi kuilaumu serikali peke yake mana hilo ni zao la Wapiga kura wengi ambao pia wana ubinafsi huo huo.
Akitokea mzalendo mmoja kama Magufuli ni kumshukuru tu Mungu mana atajenga Roho ya kizalendo kwa Taifa letu na mwisho atatumia uzalendo wake kutuachia Katiba na sheria nzuri.
Usifikiri Mh. Rais haoni madhaifu yaliyopo lakini hana uwezo wa kulipinga Bunge moja kwa moja kama anavyoweza kumpinga DAS mhuni na Malaya Malaya hadharani.