Naomba nitofautiane nawe. Resources za nchi hii tunaibiwa kutokana na MIKATABA MIBOVU ambayo sisi wenyew tulisaini hasa katika kipindi cha BWM NA JK. Mmoja wa washauri na mtaalamu wa sheria za madini ni waziri katika serikali ya awamu ya tano na sita, tena ana PHD katika sheria ya Madini.
JPM alilijua hilo na hakutaka kufuta au kubadilisha mikataba hiyo akabaki akilalamika tu kuwa "Tunaibiwa sana" na kuunda tume zisizokuwa na tija yoyote ile. Alimtuma Palamagamba Kabudi apeleke muswada wa sheria bungeni ya "Kulinda raslimali za nchi", lakini cha ajabu ni kuwa sheria hiyo " HAITAHUSISHA MIKATABA ILIYOPITA". Kwa nini hakutaka au kwa nini serikali za CCM huwa hawataki kuifumua mikataba hii dhalimu? Nafikiri jibu liko wazi.
JPM angekuwa mzalendo angefumua mikataba yote ya madini, gesi na makaa ya mawe, angeanzisha soko la madini hapa hapa Tanzania na kikubwa zaidi angetengeneza Sera mpya ya madini ambayo ndiyo ingekuwa dira ya maendeleo ya sekta hiyo kwa faida ya nchi.
" Huwezi ukatatua tatizo kwa kutumia mbinu zile zile ambazo ndiyo zilizosababisha tatizo lililopo" - Albert Einstein