Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Hakuna mkwara hapo mkizingua tunahamisha hii nchi ina maeneo mengi tuu yanahitaji kujengewa chuo kikuu.
Kwa mfumo wa Afya wa nchi hii, chuo kikubwa cha Afya kinapaswa kuwepo Mbeya.

Hospitali kubwa kabisa ni Muhimbili na hapo kuna chuo tayari.

Bugando wana chuo tayari.

KCMC wana chuo tayari.

Dodoma wana Chuo tayari.

Hospitali nyingine kubwa (among top 5) ni Mbeya na ndio hiyo ina watu wa UDSM.

JK anatuamsha tu kwamba tusilete masihara kwenye mambo ya msingi, "tuwache maneno tutoe eneo"
 
[QUOTE="bagamoyo, post: 40917988, member: 209]
Ni lazima waTanzania tuwe tunafikiria na kuwaza kesho na ufanisi wa shughuli tunayotaka kuifanya, tuache roho ya umasikini kuona ekari 500 ni nyingi sana hata ikiwa ni kwa ajili ya ukulima wa mtu mmoja. Hongera mzee Jakaya Kikwete kwa kuwapa ukweli, waTanzania wenye mawazo ya uchoyo kuwa kumiliki kingi ni dhambi !

Leta master plan yenu ya mnachotaka kujenga... Jengeni hizo hamsini kwanza,tuone mtaishia wapi. Kikubwa kabisa tuhakikishieni mtapata fedha wapi za kufanya yote hayo. Tuwape 500 ama 1000 Halafu eneo likae miakia hamsini halijaendelezwa, hilo halikubaliki.
[/QUOTE]
Lakini niulize swali? hicho chuo kinataka kulima au kufundisha wanafunzi? hivi kweli unahitaji hekali 500 za chuo kwa ajiri ya nini? Pale Dar sidhani hata kama zinafika hizo hekali 1000 na zimewashinda wameanza wamezijengea mlimani city & more are coming.
 
Hayo mashamba mtawalipa wamiliki? Hayo mabonde na milima unajua kubwa gharama za ujenzi zitakuwa juu au huelewi hilo?
Sasa mkuu, kuwalipa fidia wakulima wa Nsalaga nalo linaweza kuwa ni tatizo ?
Hayo mabonde na milima hayana shida sana.

Kwaiyo unataka mradi uende Kambikatoto kwenye vichaka vya bure huko ?

Unajua kwa mtazamo wako (wa ardhi ya kutolipa fidia, iwe tambarare, n.k) ni kwamba huo mradi hautekelezeki hata Iringa mjini, Songea mjini, Tabora, Shinyanga, Kibaha, n.k ?
 
Elewa kitu kimoja hapo Chuo kimeomba eneo serikali ya mkoa inatafuta eneo ambalo hawataingia gharama za kulipa, ingekuwa chuo chenyewe kinataka eneo fulani maana yake kingekuwa na fedha ya kuwalipa wahusika fidia ili waondoke
 
Unadhani serikali ya mkoa ina eneo ambalo italipata bure ?
 
Naunga Mkono Kikwete Kaona Mbali
Mbeya hakuna eneo la wazi la ukubwa huo labda Ihefu au wabadilishe matumizi ya mashamba ya chai kule Rungwe,kwa ufupi Mbeya imeshonana.maeneo yaliyo wazi ni ama hifadhi za misitu au mashamba ya chai au makambi ya majeshi yetu.
 
Muhimu wasilazimishe kutafuta hizo hekari 500 kwa kuwapora wanyonge ardhi yao, wakitaka kuzipata wawe tayari kuwalipa fidia wote watakaoathirika na hili wazo la Kikwete.

Sioni sababu kwanini wasijenge vitu vichache vya msingi kwa eneo lililopo, hizo nyumba za wahadhiri, hosteli, na hospitali vinaweza kuwa sehemu nyingine bora pasiwe mbali sana na chuo, kuliko kulazimisha vyote viwe pamoja kama chuo kimekuwa mbuga ya wanyama.
Kama ilivyokwa Muhimbili na Mlonganzila, Mbeya hakuna ardhi ya bure ya hizo ekari nyingi.
 
Yuo sahihi sana. Viongozi wa Tanzania, walio wengi uwezo wao wa kufikiri unaishia miaka mitatu. Hawafikrii miaka 50 au 100 ijayo, kama chuo kitataka kuongeza majengo, hizo ekari 50 zitakidhi hitaji hilo.
UDOM majengo yamekuwa makazi ya popo,kwanini chuo kiwe na eneo kubwa kiasi hicho wakati ni baadhi tu ya vitivo vitakuwa hapo, tungejifunza kutoka ujenzi wa UDOM na maumizi yake
 
Ni hivi kisheria Ardhi inamilikiwa na kijiji/mtaa, halamshauri husika hivyo ukienda mkoani RAS anamwandikia mkurugenzi wa halamshauri husika atafute hiyo ardhi sawa kijana nakutakia usiku mwema
Kijiji hakiwezi kukupa ardhi zaidi ya hekta 250 au hekta 100.
 
Back
Top Bottom