Rais Mwinyi awakabidhi vyeti vya uraia wa Tanzania wahamiaji wasiohamishika 3,319

Rais Mwinyi awakabidhi vyeti vya uraia wa Tanzania wahamiaji wasiohamishika 3,319

uzanzibari au uraia wa Tanzania, kwanini asiwe Samia ndio wa kutoa vyeti hivyo? yeye ana mamlaka gani kwa Tanzania?
Mwinyi ni Mzanzibara harafwu hao warundi wa burundi na rwanda ni jamaa zenu ,hilo kwenu jipya ila Zanzibar wapo mpaka wachina ambao ni raia wa Tanzania visiwani,tena Pemba mjini Mkowani na wapo wanaishi na wenyeji vizuri tu,
Unguja wapo wachina ukisikia wachina Tambi wapo tokea enzi za ukombozhi.

Ndio waZhanzhibari wakadai moja ya madai yao Raisi wa Zanzibar awe makamo wa kwanza wa Raisi,ila mmepangua kwa sababu mnazozitaka nyinyi na waZanzibari nao sasa wamekuja na kali zaidi,
Chaguweni Raisi wa Tanzania kila uchaguzi kutoka Tanganyika, (sawa sawa) by Tundu Lisu.
Wazenji wakifanya ya kufanya Raisi wenu kutoka Tanganyika hamalizi miaka mitatu wazenji wanarithi Uraisi.
Endeleeni na ubaya wenu wa kutompa nafasi Mzanzibari kugombea nafasi ya Uraisi wa Tanzania ,mjue mtakaemchagua anakalia kuti kavu.
 
Tanzanian tumekuwa wapumbavu na washamba WA mambo ya kiulimwengu .Tumekuwa wabinafsi Kila kitu kusingizia ccm.! Sasa watu kupewa uraia Kuna ajabu gani wazeee acheni basi ushamba.

Wa Africa kibao wanapewa uraia nchi za watu na maisha yanasonga iweje kwetu tuanze kutiana Hila ??

Ubelgiji hapo Kuna wakongo kibao ,warundi kibao,

Race nyeusi za kutosha ulaya.

Ila hapo Zanzibar tu waafrica wenzetu tena ambao wamezaliwa hapa hapa mnaleta chuki na kuwasema wazanzibar
 
mpumbavu ni wewe peke yako ndugu, usitujumuishe na sisi.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema nchi imeandika historia mpya kwa kuwakabidhi vyeti vya uraia wa Tanzania wahamiaji wasiohamishika 3,319 ambao wameishi nchini kwa zaidi ya miaka 50 wakiwa na asili ya mataifa jirani ya Burundi, Comoro, Msumbiji na Rwanda.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo leo tarehe 05 Septemba 2023 katika hafla ya kukabidhi vyeti vya uraia wa Tanzania kundi la Wahamiaji wasiohamishika Ikulu, Zanzibar.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amefurahishwa kutekelezwa ahadi yake aliyoitoa baada ya kuingia madarakani mwaka 2020 kwa kumalizika zoezi hilo na kuwafanya watambulike kuwa Raia wa Tanzania badala ya Wahamiaji wasiohamishika.

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa Idara ya Uhamiaji nchini kuziimarisha sheria zilizopo hususani sheria ya uraia wa Tanzania kwa kuwa sheria hii haijafanyiwa mapitio kwa kipindi kirefu kwa madhumuni ya kuiwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowahusu wananchi na wageni wanaofika nchini.

View attachment 2739721
Suala la uhamiaji ni suala la muungano ambalo mwenye mamlaka nalo ni rais wa JMT inakuwaje rais wa Zanzibar atoe hadhi uraia kwa raia wasiohamishika? Kama rais wa Zanzibar ana mamlaka ya kutoa uraia wa wahamiaji wasiohamishika ndio maana Wabara wanahamasika kudai Tanganyika hamna namna ya kukwepa hapo tayari imeingia kwenye rekodi rejea (Case Study)
 
Hivi Rais wa Zanzibar anatoa vipi Uraia wa Tanzania?

Something is wrong! Rais wa Zanzibar anakuwaje na Mamlaka kwa mambo ya Tanzania?

Hao aliowapa Uraia wa Tanzania ni kwa ajili ya kuishi Tanganyika, Mwinyi hatawapa vitambulisho vya Mzanzibar Mkaazi
 
Kwa Tanzania yeye ni makamu wa kwanza wa Rais, yuko juu ya makamu wa Rais kiitifaki. Pia ni miongoni mwa wajumbe wa baraza la mawaziri, na anafanya kazi yoyote alivyoagizwa na Rais wa Tanzania nzima.
Kimamlaka anaanza Rais, anakuja Rais wa Znz halafu ndio makamu wa Rais
Unawazimu. Katiba iliyopo huyu ni mjumbe tu wa baraza la mawaziri. Anaapa kwa raisi wa Jamhuri kutunza siri za baraza la mawaziri. Amepewa tu precedence kwenye itifaki. Makamu wa Raisi wa Tanzania haapi kwa raisi bali anaapa kwa Jaji mkuu. Kuna tofauti kubwa sana hapo.
 
Hivi Rais wa Zanzibar anatoa vipi Uraia wa Tanzania?

Something is wrong! Rais wa Zanzibar anakuwaje na Mamlaka kwa mambo ya Tanzania?

Hao aliowapa Uraia wa Tanzania ni kwa ajili ya kuishi Tanganyika, Mwinyi hatawapa vitambulisho vya Mzanzibar Mkaazi
Ndo maana inabidi tuidai Tangangika kwa nguvu. Either tuwe nchi moja na serikali moja au kila mtu apite na vyake. Hatuwezi kufanya kuku wa mnadani kila siku au mbuzi wa kafara.
 
T

Tumia akili yako VIZURI, ingekuwa hivyo angemrithi magufuli.
Hakunrithi Magufuli kwasababu katiba inataja nani anarithi Rais. Ila pia katiba hiyohiyo kiitifaki inamuweka Rais wa Znz juu ya makamu wa Rais wa muungano
 
Hivi Rais wa Zanzibar anatoa vipi Uraia wa Tanzania?

Something is wrong! Rais wa Zanzibar anakuwaje na Mamlaka kwa mambo ya Tanzania?

Hao aliowapa Uraia wa Tanzania ni kwa ajili ya kuishi Tanganyika, Mwinyi hatawapa vitambulisho vya Mzanzibar Mkaazi
Hivi unajua wazanzibari uraia wao ni Tanzania, kile kitambulisho cha Zanzibar sio citizenship ID ama national ID kile ni residence ID kazi yake ni kutambulisha tu fulani bin fulani ni mkazi wa Zanzibar, hakisemi raia wa Zanzibar kinasema mkazi wa Zanzibar, maana uraia wa Wazanzibar unaitwa Tanzania. Hebu punguzeni kujaza misuli ya mafuvu muelewe basi
 
Sikiliza ndugu, hayo yote tunayajua na kuna sababu za ID ya Wazanzibar kuwa Tanzania.
Sababu kubwa ni ili wakija Bara waweze kupata huduma na fursa sawa na Watanganyika.

Katika kubagua , wameweka kitambulisho cha Uzanzibar Ukaazi. Hiki maana yake ni kwamba 'fulani ni Mzanzibar' hivyo anaweza kupata ardhi, ajira za SMZ , kupiga kura, kama ni kijana kupata ZHESLB n.k.

Mtu wa Bara kwa kitambulisho cha Utanzania hawezi kupata fursa zile zile za Mzanzibar Mkaazi.

Kwahiyo Wanautaka Utanzania si kwa mapenzi ni kwa mafao, na wana ubaguzi kwa Watanzania kwasababu ya kitambulisho cha Uzanzibar ukaazi

Hao wakimbizi hawatapewa kitambulisho cha Uzanzibar Ukaazi bali Utanzania ili waweze kuhamia Bara lakini ikionekana wamepokelewa Zanzibar. Mbinu hizi za kitoto trunazijua sana kwahiyo hawawezi kutubabisha.
Tunajua kinachoendelea sasa hivi kati ya Familia za Urais! I

Nitajie Rais Mwingine wa Zanzibar aliyewahi kutoa Uraia baada ya mwaka 1964.
 
Kwa Tanzania yeye ni makamu wa kwanza wa Rais, yuko juu ya makamu wa Rais kiitifaki. Pia ni miongoni mwa wajumbe wa baraza la mawaziri, na anafanya kazi yoyote alivyoagizwa na Rais wa Tanzania nzima.
Kimamlaka anaanza Rais, anakuja Rais wa Znz halafu ndio makamu wa Rais
Rais WA znz ni mtu WA tano Sasa kimamlaka...akianza na Rais JMT, Makamu wake,waziri mkuu na naibu wake kisha ndio yeye
 
Tanzanian tumekuwa wapumbavu na washamba WA mambo ya kiulimwengu .Tumekuwa wabinafsi Kila kitu kusingizia ccm.! Sasa watu kupewa uraia Kuna ajabu gani wazeee acheni basi ushamba.

Wa Africa kibao wanapewa uraia nchi za watu na maisha yanasonga iweje kwetu tuanze kutiana Hila ??

Ubelgiji hapo Kuna wakongo kibao ,warundi kibao,

Race nyeusi za kutosha ulaya.

Ila hapo Zanzibar tu waafrica wenzetu tena ambao wamezaliwa hapa hapa mnaleta chuki na kuwasema wazanzibar
Umenyoosha maelezo
 
Wazanzibar waletwe bara, na wabara wapelekwe zanzibar, ili zanzibar iwe nzuri ni lazima wabara waingie na kufanya 50%, alkadhalika Wazanzibar waje bara na kupewa privilege maalum, ili utaifa wetu usimame na kuondoa rabsha.
 
Tanzanian tumekuwa wapumbavu na washamba WA mambo ya kiulimwengu .Tumekuwa wabinafsi Kila kitu kusingizia ccm.! Sasa watu kupewa uraia Kuna ajabu gani wazeee acheni basi ushamba.

Wa Africa kibao wanapewa uraia nchi za watu na maisha yanasonga iweje kwetu tuanze kutiana Hila ??

Ubelgiji hapo Kuna wakongo kibao ,warundi kibao,

Race nyeusi za kutosha ulaya.

Ila hapo Zanzibar tu waafrica wenzetu tena ambao wamezaliwa hapa hapa mnaleta chuki na kuwasema wazanzibar
Hahaha mi nasema mijitu ya bara ni washamba na wezi,wanajifanya wazalendo kisa kazaliwa porini huko na kukulia kwenye shida. Watu wa bara ukiachana na wapwani wengi hawana exposure hata asome vipi. Watu washamba sana Tanzania ila tatizo ni elimu walinyimwa toka zamani.
 
Hii ni 2023 ila still na elimu yote iliyokua mtandaoni Bado watu kisa kazaliwa porini na kasoma Kwa shida anajiona yeye ni mzalendo na Tanzania na serikali yake itamuokoa. Yaaani mtu hajui Dunia inabadilika na utandawazi hauwezi kushindana nao ila mtu anaona uraia wa Tanzania ni bonge la dili kiasi anakua mbaguzi na kukuona yeye ndio Bora.

Nyie watu wa porini acheni ushamba mnataka maendeleo ila hamtaki effects za kuendelea.
 
Rais wa Zanzibar hachaguliwi na Mtanganyika na hana mamlaka na jambo lolote la Tanganyika.

Rais wa Zanzibar anapotoa Uraia kwa watu anawapa haki ikiwemo ya kumiliki Ardhi huku Tanganyika.

Ni Rais Mwinyi huyo huyo anayesema Mtanganyika anamilikishwa ardhi kama mgeni kule Zanzibar.

Nadhani Rais SSH kuna mahali anaifikisha hii nchi, na 'bomu' siku likilipuka hakuna Nyerere wa kulizima kama G55.

Tusipokuwa makini nchi itauzwa, itamwegwa itafanyiwa kila hila, kwani wao wana nini cha kupoteza?
Nchi itauzwa wewe ya kwako?au kisa umezaliwa porini huko tayari ushamilikisha nchi nakuona wengine sio wazalendo na hawajui?
 
Uraia wa Tanzania kuna watu wanautamani ila kuna vijana wavuta bangi utasikia anakwambia bora azaliwe mbwa marekani.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Ukitokea kwenye zile Major Cartels za CCM lazma uutamani. Ila kwa mbwa kachoka saga na rumba wa kitaani ni mzigo mzito.

Ingewezekana kuingia ubia wa uraia mtu awekeze na afanyie bizness NIDA yangu kisha anilipe nisingepoteza hata Nukta.
 
Back
Top Bottom