Rais Mwinyi hapa umekosea sana, ‘contractors bashing’ unaifanya sehemu ya siasa

Rais Mwinyi hapa umekosea sana, ‘contractors bashing’ unaifanya sehemu ya siasa

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Nimesikitishwa na kauli za Rais wa Zanzibar juu ya mkandarasi aliyekuwa akijenga jengo la serikali huko Zanzibar.

Mwinyi naona kaingiza siasa kwenye kazi za kitaalam isivyo.

Kwa muonekano tu Mkandarasi na Consultant wanatoka Bara.

Sababu za kuwafuta hiyo contract haziko wazi, lakini tokana na maelezo ya Rais, ni mkadarasi kuomba kuongezewa muda kwa miezi sita!

Na Consulant eti alitakiwa kuongea kile Rais anapenda kusikia!

Ajabu sana hii. Nani asiyejua Zanzibar hakuna kokoto wala cement , wala mchanga, VYOTE VINATOKA BARA.

Kwa msimamo kama huu kwa nini makandarasi wa SGR na wale wa Bwawa la Umeme JNHP-Stieglers wasisimamshwe?

Tunaona kuna element ya siasa za Uzanzbari katika hili.

Itategemeana na terms walizosaini kwenye mkataba walioingia kati ya serikali na mkandarasi.

Mambo ya dharura yanatakiwa kuzingatiwa, usafiri nk. Kama serikali imevunja mkataba akawashtaki adai fidia.
 
Umeandika ujinga mtupu! Hayo yote hayakuwekwa kwenye plan na timeline ya mkandarasi haikuconsider kuhusu mchanga kutoka bara?
Watu mlio na akili ndogo ndogo na wenye vijumba vya nyasi, akili zenu vigumu kuelewa kwa nini hata SGR na Stiglaz bado ziko nyuma ya wakati kukamilika.
 
Makadarasi walikuwa na mikutano Dodoma.
Wameshangazwa sana na hli tukio.
Clip imetembea sana.
Kuna waliofedheheshwa sana na kitendo hiki.
 
Kwanini unaleta ubara na uvisiwani kwenye ishu za uzembe wa mkandarasi. Ndio maana mashabiki wa mwendazake mnaonekana hamnazo na wabaguzi.
 
Nimesikitishwa na kauli za Rais wa Zanzibar juu ya mkandarasi aliyekuwa akijenga jengo la serikali huko Zanzibar.
Mwinyi naona kaingiza siasa kwenye kazi za kitaalam isivyo.

Kwa muonekano tu Mkandarasi na Consultant wanatoka Bara.

Sababu za kuwafuta hiyo contract haziko wazi, lakini tokana na maelezo ya Rais, ni mkadarasi kuomba kuongezewa muda kwa miezi sita!
Na Consulant eti alitakiwa kuongea kile Rais anapenda kusikia!

Ajabu sana hii.
Nani asiyejua Zanzibar hakuna kokoto wala cement , wala mchanga, VYOTE VINATOKA BARA.

Kwa msimamo kama huu kwa nini makandarasi wa SGR na wale wa Bwawa la Umeme JNHP-Stieglers wasisimamshwe?

Tunaona kuna element ya siasa za Uzanzbari katika hili.
View attachment 2294254
Inasikitisha!
Hapo utawala bora kufuata mkataba inasemaje?
Angefanya hivyo an inexperienced admnistrator kama Sabaya tungeelewa.

zlakini kwa Rais aliyekuwa katika serikali ya muungano kwa miaka 20 kutofuata hatua za termination of contract, inaficha udhaifu wa mtu.
 
Back
Top Bottom