Nchi hii ina watu wa mirengo minne.Kuna wajamaa maslahi ,wajamaa maendeleo, mabepari Wezi na mabepari wabinafsi.
Lakini pia katika kutekeleza Sera na mipango panaibuka makundi mawili.
Kundi la wasomi walioandaliwa kwa karne nyingi na wakoloni kwa ajili ya kuwa vibaraka wa ukoloni na kudumisha mila za wakaloni. Hawa hawajali shughuli za kujiajiri wanazofanya wafanyabiashara. Hawa kazi yao ni kukimbilia madaraka ,vyeo, ajira ili wapate madili mbalimbali,rushwa na kila aina ya utapeli kwenye maofisi ya umma. Hawa ndio wanaokwamisha wawekezaji,wafanyabiashara na miradi ya umma kuendelea. Hawa sio wazalishaji wala waajiri bali ni watumbuaji wa kodi za wananchi kupitia ofisi za umma.
Wanajitahidi sana kusoma na kuwa na vyeti vikubwa vikubwa sio kwa sababu ya kuongeza ufanisi wa kazi na utendaji zaidi Bali kupata mishahara mikubwa na marupurupu mengi ili waongeze nyumba ndogo na kujazana kwenye mabaa na mahoteli kwa ufuska.
Hawa ni tatizo sana kwa miaka mingi. Hawa hawajui changamoto za wafanyabiashara zaidi ya kuwaza kuwakomoa wafanyabiashara na kuwaumiza kwa Kodi ili wao waendelee kupata mashlahi huku wenzao ambao ni wafanyabiashara wakiwa wanafilisika. Hawa wao wanafurahia wanaposikia kuwa mipaka imefungwa na bidhaa kutoka na kuingia haziwezi kupita. Wanafurahia na kusifia kuwa ni njia ya kuwakomesha wafanyabiashara.
Kundi lingine ni lile la Wafanyabiashara. Hawa sio wasomi wa uchumi wa kwenye virabu vya wakoloni. Hawa ni wafanyabiashara kwa vipaji vyao vya kuzaliwa . Hawa ni watu wanaojiajiri wenyewe na kuajiri wengine. Lakini wanapata mazingira magumu sana kutokana na kundi lile la waajiriwa,watendaji,wasomi waliokalia madaraka na maofisi ya umma.
Biashara ni kazi kubwa sana ya kiuchumi tangu enzi na enzi. Kazi halali kwa binadamu kwa karne nyingi ni Kilimo ,ufugaji, uvuvi na Biashara. Hizi kwa Afraika zinaonekana kama kazi za watu wasio na elimu ndio maana kundi kubwa la wasomi wanazikimbia huku wakijazana kwenye kutafuta ajira za mishahara ya mwisho wa mwezi. Matokeo yake wanapoona mishahara haiwezi kutosha wanajihusisha na wizi. Kundi hili limetapakaa kwenye siasa pia.
Familia hizi mbili za wanaoamini katika usomi wa kikoloni wa kuajiriwa na ile ya biashara kwa ajili ya vipato zinapofanikiwa kuwa na kiongozi anayetokana na imani hizo basi ndivyo na nchi itakavyokwenda .
Hongera Hussein Mwinyi kwa kuziona changamoto za wafanyabiashara.
Biashara zinahitaji imani kubwa mana ni watu wanaojiajri wenyewe na kuajiri wengine. Wanajitegemea kwenye gharama za afya. Wanajitegemea kwenye kulipa Kodi,wanajitegemea kulipa Huduma za afya, wanajitegemea kwenye mawasililano ,wanajitegemea kwenye usafiri,wanajitegemea kwenye makazi n.k. Tofauti na mabosi wasomi na watawala maofisini wanaogharamikiwa na umma kwa mambo mengi.
Hata hivyo Mh. Dr. Mwinyi atafakari mfumo wa serikali yake ya mapinduzi ,mana kuna watumiaji wa pato la taifa wengi kuliko wazalishaji.
Serikali na mifumo yake inatumia sehemu kubwa sana ya pato la nchi kwa mambo ya kiutawala na siasa.