Rais Mwinyi: Watu wanadhani kuweka kodi kubwa ndio pato kubwa kwa Serikali, kodi kubwa inapunguza wafanyabiashara

Rais Mwinyi: Watu wanadhani kuweka kodi kubwa ndio pato kubwa kwa Serikali, kodi kubwa inapunguza wafanyabiashara

Msisahau hata Baba lao aliposhika Kijiti 2015 Tulitoa sifa kedekede.
muda utasema.
ni vyema kuwa neutral.
 
Amesomea udaktari lakini anajua basic principles za biashara; huu ni mwanzo mzuri ili mradi asiwasikilize wachumi uchwara toka bara wanaodhani kwa kuweka kodi kubwa ndio watakusanya mapato zaidi!!!
 
Nchi hii ina watu wa mirengo minne.Kuna wajamaa maslahi ,wajamaa maendeleo, mabepari Wezi na mabepari wabinafsi.

Lakini pia katika kutekeleza Sera na mipango panaibuka makundi mawili.
Kundi la wasomi walioandaliwa kwa karne nyingi na wakoloni kwa ajili ya kuwa vibaraka wa ukoloni na kudumisha mila za wakaloni. Hawa hawajali shughuli za kujiajiri wanazofanya wafanyabiashara. Hawa kazi yao ni kukimbilia madaraka ,vyeo, ajira ili wapate madili mbalimbali,rushwa na kila aina ya utapeli kwenye maofisi ya umma. Hawa ndio wanaokwamisha wawekezaji,wafanyabiashara na miradi ya umma kuendelea. Hawa sio wazalishaji wala waajiri bali ni watumbuaji wa kodi za wananchi kupitia ofisi za umma.

Wanajitahidi sana kusoma na kuwa na vyeti vikubwa vikubwa sio kwa sababu ya kuongeza ufanisi wa kazi na utendaji zaidi Bali kupata mishahara mikubwa na marupurupu mengi ili waongeze nyumba ndogo na kujazana kwenye mabaa na mahoteli kwa ufuska.
Hawa ni tatizo sana kwa miaka mingi. Hawa hawajui changamoto za wafanyabiashara zaidi ya kuwaza kuwakomoa wafanyabiashara na kuwaumiza kwa Kodi ili wao waendelee kupata mashlahi huku wenzao ambao ni wafanyabiashara wakiwa wanafilisika. Hawa wao wanafurahia wanaposikia kuwa mipaka imefungwa na bidhaa kutoka na kuingia haziwezi kupita. Wanafurahia na kusifia kuwa ni njia ya kuwakomesha wafanyabiashara.

Kundi lingine ni lile la Wafanyabiashara. Hawa sio wasomi wa uchumi wa kwenye virabu vya wakoloni. Hawa ni wafanyabiashara kwa vipaji vyao vya kuzaliwa . Hawa ni watu wanaojiajiri wenyewe na kuajiri wengine. Lakini wanapata mazingira magumu sana kutokana na kundi lile la waajiriwa,watendaji,wasomi waliokalia madaraka na maofisi ya umma.

Biashara ni kazi kubwa sana ya kiuchumi tangu enzi na enzi. Kazi halali kwa binadamu kwa karne nyingi ni Kilimo ,ufugaji, uvuvi na Biashara. Hizi kwa Afraika zinaonekana kama kazi za watu wasio na elimu ndio maana kundi kubwa la wasomi wanazikimbia huku wakijazana kwenye kutafuta ajira za mishahara ya mwisho wa mwezi. Matokeo yake wanapoona mishahara haiwezi kutosha wanajihusisha na wizi. Kundi hili limetapakaa kwenye siasa pia.


Familia hizi mbili za wanaoamini katika usomi wa kikoloni wa kuajiriwa na ile ya biashara kwa ajili ya vipato zinapofanikiwa kuwa na kiongozi anayetokana na imani hizo basi ndivyo na nchi itakavyokwenda .

Hongera Hussein Mwinyi kwa kuziona changamoto za wafanyabiashara.

Biashara zinahitaji imani kubwa mana ni watu wanaojiajri wenyewe na kuajiri wengine. Wanajitegemea kwenye gharama za afya. Wanajitegemea kwenye kulipa Kodi,wanajitegemea kulipa Huduma za afya, wanajitegemea kwenye mawasililano ,wanajitegemea kwenye usafiri,wanajitegemea kwenye makazi n.k. Tofauti na mabosi wasomi na watawala maofisini wanaogharamikiwa na umma kwa mambo mengi.

Hata hivyo Mh. Dr. Mwinyi atafakari mfumo wa serikali yake ya mapinduzi ,mana kuna watumiaji wa pato la taifa wengi kuliko wazalishaji.
Serikali na mifumo yake inatumia sehemu kubwa sana ya pato la nchi kwa mambo ya kiutawala na siasa.
 
Ilitakiwa na azam tv wangekuwa namaono haya wanawaza kupandisha bei matokeo wataomba kuzifungia chaneli zabure kwani kisimbuzi chao watakao lipa niwachache kuliko watakao kuwa wanatumia kwa chaneli zabure
 
Nan amekomolewa? kudai kodi za nyuma sio kukomoa
Ati kudai kodi za nyuma!
Ujinga TRA hauishi.
Wanavyofanya ndio njia ya wazi kukimbiza biashara, na sasa wameanzisha mtindo wa kublock na kuchukua-kupora fadha benki.
Hapo nani atawekeza?
Sheria za Kodi-TRA hata wao wenyewe hazielewi.
Kiufupi biashara zinafilisiwa mchana kweupe kwa kisingizio cha kodi cha nyuma.
 
Nilishasema, huyu ndiye next President wa URT...

Angalia haya maneno yake then angalia na hali yetu huku bara.. Huyu atakuja kuonekana kama masia 2025 na kuungwa mkono na kundi kubwa tu na atashinda bila hata mbeleko ya Polisi na NEC..
 
Kanaonekana kuwa na busara haka kajamaa kuzidi lile dubwasha eeeh?
Sasa kijana ameishi ikulu 10 yrs, baba yake amekuwa waziri many years, kashika nyazifa nyingi strategically, alipata elimu nje ya nchi na ma exposure kibao, ni Mtoto wa mjini anaejua kula bila kufanya majungu + hekima za Mzee ruksa na Mzee Kikwete kwamba umeingia kwa nguvu lakini watendee watu haki ili wasikumbuke dhulma walotendewa ya kuporwa uchaguzi
 
Nilishasema, huyu ndiye next President wa URT...

Angalia haya maneno yake then angalia na hali yetu huku bara.. Huyu atakuja kuonekana kama masia 2025 na kuungwa mkono na kundi kubwa tu na atashinda bila hata mbeleko ya Polisi na NEC..
2025!!??
 
Msisahau hata Baba lao aliposhika Kijiti 2015 Tulitoa sifa kedekede.
muda utasema.
ni vyema kuwa neutral.
Watanzania ,watanganyika na wazanzibar wanakatishwa tamaa na baadhi ya wanasiasa na maamuzi yao, hivyo wanaamua kuachana na mambo ya kufatilia Siasa!

Niwakumbushe tu ndugu zangu, sukari tunayokorogea Hot beverage ni siasa, mafuta tunayoweka kwenye automobile ni siasa, beer na condom tunazotumia ni siasa!

Tusiache, tuendelee kujadili SIASA, siasa ni maisha.
 
Nahamishia biashara zangu Zanzibar naona tunaendana kihekima na huyu Rais mwerevu... Bye bye Dar-es-salaam nlikupenda lakini ntakupenda tena 2025 wateja bidhaa nitatuma msijali
Usijali atotoka mtarudi nyote mliokimbia kufilisiwa tujenge nchi
 
Mtoto wa kishua huyooooo!, hana shida na watu, anawataka wapate wote duuu!. anafanya km Baba yake mzee Rhuksa! jamani kweli mtoto wa Nyoka ni nyoka.

Mitoto ya Mazogoroni bwana weee! ina chuki hiyo mara nilisomea kibatari, mara nilinunuliwa kaptura ya shule na mzee wa kjiji. saa ngapi? anachukia hata wafuga mbwa!

J. Kikwete angeongoza na huyu TZ ingekuwa km Ulaya.

Wazungu wana akili sana hawa huenda ni miungu kweli, wao km hujawahi kuishi ushuani, Maisha ya kula nz kusaza hupewi kiti cha Urais! utaleta utopolo tu! unafurahia shida. mimi nahamia zanzibar Rasmi niitwe chogo sawa tu ntavumilia!
 
Nahamishia biashara zangu Zanzibar naona tunaendana kihekima na huyu Rais mwerevu... Bye bye Dar-es-salaam nlikupenda lakini ntakupenda tena 2025 wateja bidhaa nitatuma msijali
Labda huwajui wazanzibar wewe! Nenda uone.
 
Mzee jazia nyama kuhusu Texas. Mh. Mwinyi yupo humu anakusoma.
Anajua namna ya kupata hizo sheria na hata singapore wanatumia sheria zinazofanana na Texas kwenye masuala ya kodi na uwekezaji na mazingira ya singapore ni sawa na ZNZ ila ZNZ ni mazuri zaidi, hivyo ni uamuzi wake kuifanya masikini au Tajiri.
 
Back
Top Bottom