Rais na Mwenyekiti wangu, usisubiri mpaka uharibifu wa Spika Ndugai ukuchafue

Rais na Mwenyekiti wangu, usisubiri mpaka uharibifu wa Spika Ndugai ukuchafue

Imefikia hatua Spika anamkosoa kila lililo jema na kukubali yasiyofaa. Ukosoaji wa namna hii si afya kwa ustawi wa nchi yetu.

Tabia hii ameanza kuonesha katika hiki cha awamu ya sita. Mbona Rais Magufuli alikuwa anafanya yanayofanywa na awamu hii lakini hakuwahi kukosoa?

Ukosoaji wa aina ya Ndugai ni moja wa ufa hatari sana katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi. Ukiachana na nchi chache sana duniani ambazo zina uchumi imara wa kujiendesha zenyewe, nchi nyingi zinategemea mikopo ili kukamilisha ujenzi.

Spika licha ya kujua umuhimu wa mikopo yenye riba nafuu na masharti rahisi lakini bado anaona mikopo hiyo haifai. Bila kutoa njia mbadala wa kuongeza mapato ya ndani anapinga mikopo nafuu. Je, maendeleo yatakujaje?

Yawezekana Spika kaona siku zake za kukalia kiti cha uspika zimeisha au ana nia na lengo tofauti la kumkwamisha Rais na Mwenyekiti wake.

Rais na Mwenyekiti wangu, nguvu na uwezo wa kumtoa Spika unao, fanya sasa kabla uharibifu wa Spika haujaota mizizi itakayokuwa migumu kuing'oa
Hivi Rais anaweza akatumia mbinu au sheria ipi kumtoa huyo mgogo ndugai, kwakweli Ni msaliti
 
2025 tutashuhudia mengi. Naona Samia nae kaonyesha misuli yake. Kasema ataendelea kukopa. Ila sasa kama wanakopa hizi tozo zetu zinafanya kazi gani ?Au ndo zinawalipa allowances za safari zao.
Mrudi shule nyie sukuma Gang, kwaiyo hizo zetu ndio zitatosha kukamilisha hiyo miradi yote au, mbona msukuma mwenzenu dikteta kwa miaka yake mitano amekopa trillion 30, hamkuwa mkipiga kelele wapuuzi nyie
 
Serikali yenye akili husisitiza uzalishaji wa ndani ili iweze kuuza nje na kupata fedha za kigeni. Wanaompotosha mama kwa kopa kopaa kopaaaa kopaaaaaa kopaaaa@aaaaaaaq, sijui wana maana gani.
Tukope kwa tahadhari na kwa viwango.
Sasa haya maneno mngemwambia msukuma mwenzenu kipindi kile,maana yeye ndio amevunja rekodi ya kukopa, kwa miaka 5 tu kakopa trillion 30
 
Mnacheza ngoma ya CCM! CCM mtu hawezi kuongea bila kujua Mkiti anataka nini, Ndugai ni mjumbe wa kamati kuu ya chama, na ni spika, anaaccess ya moja kwa moja na Rais, na sidhani kama inapita wiki moja bila kuongea na Rais! Unadhani anajiongelea tu bila kujua nini anafanya/wanafanya?
Hakuna spinning inayo deteriorate image ya mtu na kutishia uhai wa cheo chake.Stop overthinking.
 
Ni kweli japo nampinga ndugai kwa unafiki wake lkn matokeo ya madeni huwa ni mabaya.
Haya ni matokeo ya uharamu wa utawala wa ccm
 
Kwa hiyo samia naye anajibu bila kujua nn anajibu???
... kwendraaaa zako
Hakuna spinning inayo deteriorate image ya mtu na kutishia uhai wa cheo chake.Stop overthinking.
 
Hivi Rais anaweza akatumia mbinu au sheria ipi kumtoa huyo mgogo ndugai, kwakweli Ni msaliti
Mbona ni rahisi tu,Kamati ya maadili kumnyang'anya uanachama.anakuwa amekosa sifa zote,tena wasichelewe kumvua.
Ushauri kwa Mama.
Piga chini ndugai,
Naibu asipewe uspika,
Simamia katiba mpya kabla 2025.
Usijaribu 2025 kuchukua fomu 2025.
Utabaki na heshima kubwa yenye historia kizazi na kizazi.
 
Kwani mwenye nguvu za kumwondoa mwenzake ni nani? hebu wajuvi njooni mdadavue hapa......
 
Acha uzushi na propaganda za kijinga, takwimu za kukopa hiyo trillion 10, umezitoa wapi? Deni la Taifa hadi Sasa no trillion 72. Magufuli aliacha deni la Taifa likiwa trl.71, Kiwete aliacha likiwa trl.43. Kama Samia angekuwa kakopa trl.10 Kama unavyo dai deni Taifa lingekuwa trl 80+.
Deni la taifa kwa Sasa ni trillion 82, chukua hiyo
 
Lakini mikopo ni hatari. Serikali inayosisitiza kukopa sio serikali ya kuishabikia hata kidogo. Sera zako za kiuchumi zitavurigika sana kama utategemea uchumi. Itafika mahali sera za kiuchumi utapangiwa ili uwezw kuserve debt.
bongo bwana utafikiri tumejichagua kukaa pamoja.wabunge wasipo kosoa mnasema wanapiga makofi tu.wakikosoa mnasema hawaitakii mema taifa.sasa tusimamie wapi
 
Imefikia hatua Spika anamkosoa kila lililo jema na kukubali yasiyofaa. Ukosoaji wa namna hii si afya kwa ustawi wa nchi yetu.

Tabia hii ameanza kuonesha katika hiki cha awamu ya sita. Mbona Rais Magufuli alikuwa anafanya yanayofanywa na awamu hii lakini hakuwahi kukosoa?

Ukosoaji wa aina ya Ndugai ni moja wa ufa hatari sana katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi. Ukiachana na nchi chache sana duniani ambazo zina uchumi imara wa kujiendesha zenyewe, nchi nyingi zinategemea mikopo ili kukamilisha ujenzi.

Spika licha ya kujua umuhimu wa mikopo yenye riba nafuu na masharti rahisi lakini bado anaona mikopo hiyo haifai. Bila kutoa njia mbadala wa kuongeza mapato ya ndani anapinga mikopo nafuu. Je, maendeleo yatakujaje?

Yawezekana Spika kaona siku zake za kukalia kiti cha uspika zimeisha au ana nia na lengo tofauti la kumkwamisha Rais na Mwenyekiti wake.

Rais na Mwenyekiti wangu, nguvu na uwezo wa kumtoa Spika unao, fanya sasa kabla uharibifu wa Spika haujaota mizizi itakayokuwa migumu kuing'oa
Yake ya Marehem Sita Lowasa yameanza. Ndugai(sita) lazima genge lileee linahusika
 
Mrudi shule nyie sukuma Gang, kwaiyo hizo zetu ndio zitatosha kukamilisha hiyo miradi yote au, mbona msukuma mwenzenu dikteta kwa miaka yake mitano amekopa trillion 30, hamkuwa mkipiga kelele wapuuzi nyie
Ila hakitusumbua tozo. Huyu anakopa still katuanzishia tozo. Si bora aliekuwa anakopa bila kutunyonya tena sisi.
 
Mikopo ikifanyia hizi shughuli nakuwa sina tatizo nayo! Ila kuniambia mikopo inajenga madarasa halafu tozo nazo pia zinajenga madarasa ni wizi wa mchana kweupe!

Hamnaga kitu kama hicho...Ufisadi utakuwa wa kutisha sana
Tozo za kujenga madarasa haiongelewi tena sijui imekuaje...
 
Mnacheza ngoma ya CCM! CCM mtu hawezi kuongea bila kujua Mkiti anataka nini, Ndugai ni mjumbe wa kamati kuu ya chama, na ni spika, anaaccess ya moja kwa moja na Rais, na sidhani kama inapita wiki moja bila kuongea na Rais! Unadhani anajiongelea tu bila kujua nini anafanya/wanafanya?
Naunga mkono hoja, ni gilba zao tuu
 
Back
Top Bottom