LGE2024 Rais na Viongozi wengine wa Serikali ndani ya nchi kuto kulaani mauaji yaliyofanyika kwenye Uchaguzi sio sawa

LGE2024 Rais na Viongozi wengine wa Serikali ndani ya nchi kuto kulaani mauaji yaliyofanyika kwenye Uchaguzi sio sawa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
1,012
Reaction score
2,317
Kuna mauwaji ya kigaidi yaliofanyika kwenye uchaguzi huku wengi wameuliwa kwa kupigwa risasi, lakini cha kushangaza hatuwaoni viongozi wetu wakikemea vitendo hivyo kama vile ni vizuri hii sio sawa walio kufa ni ndugu zetu sio mifugo.

Tuliona katika lile tukio la Zuchu kupigwa mawe na wananchi baada ya kuanza kumpigia kampeni Raisi Samia akiwa akitumbuiza jukwaani tuliona viongozi baadhi wakikemea kitendo hicho lakini kuhusu mauaji yaliyofanyika kwenye uchaguzi hakuna anaekemea.

Suala la mauaji ni jambo kubwa sana sio la kulifumbia macho kuliko kupigwa mawe.

PIA SOMA
-https://www.jamiiforums.com/threads/freeman-mbowe-tunalaani-mauaji-na-kujeruhiwa-kwa-wagombea-viongozi-na-wanachama-wetu-kwenye-uchaguzi-wa-serikali-za-mitaa-2024.2282025/
 
Back
Top Bottom