Nimecheka kwa nguvu huu uhuni ulioandika hapa, eti umpe fundi kandarasi ya kukujengea nyumba kisha uone anaharibu, uamue kukaa kimya mpaka amalize ndio uongee! Kumbuka yeye ni kiongozi tu, na anatawala kwa matakwa ya wananchi na sio kwamba amekabidhiwa watoto wadogo awavushe barabara.
Tumeshaumwa na nyoka. Enzi za JK tulipiga kelele kuhusu mradi wa gas kuwa kuna ufisadi ndani yake. Watetezi waliokuwa kwenye ulaji wakati huo ikiwemo Magufuli walikuwa kimya, na wengine wakitetea kama ww ulivyofanya hapa. Na lugha zilikuwa hizi hizi kuwa rais anajua kuhusu huo mradi hivyo tumuache afanye kazi. Alipoingia Magufuli anasema gas sio yetu tumepigwa na wajanja, sasa hivi yuko anajenga umeme wa maji kwa mkopo wa 6.5t ambao tuliambiwa tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi, na kundi hili hili la kina Magufuli. Halafu unataka tukae kimya kwa watu wa aina hiyo?
Unasema tumempa kazi Magufuli, kwanza hakuna uhakika kama alishinda uchaguzi, ana hata kama alishinda ni kwa kura kiasi gani. Wote tulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi, na wizi mkubwa ikiwemo mauaji na vilema hasa wapinzani. Kwa ujumla yuko madarakani kwa wizi wa kura na sio kwa ridhaa ya wananchi. Hii ndio maana anaongea kwa kushurutisha, na sio kwa ushawishi wala utaalamu wa kisayansi. Kama unamuamini muamini ww maana unafaidika na madaraka yake.