Rais ndiye kiongozi mkuu wa nchi tumempa nafasi tumwache afanye kazi yake, kelele za nini?

Sasa kama serikali haina dini kwa nini iingilie maamuzi ya viongozi wa dini kuwa sisi waumini wao tuchukue tahadhali za Corona wakati hayavunji katiba?
 
Umeandika ugolo aisee.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Kama Kibwetere alivyokuwa kiongozi basi tumfuate kama kondoo kuelekea kutuchoma moto tukiwa hai.
Tafuta ushauri wa bingwa wa maradhi ya akili
 
Ungejua kwanini kwenye jina la nchi yetu kuna neno "Jamhuri" au "Republic" usingeandika hizi pumba.



As long as Tanzania ni Jamhuri, Rais hawezi kuiongoza kama personal property.
 
Unajukumu kubwa la kuulinda uhai wako zaidi ya mtu mwingine yoyote, usipotoshwe ama kusubiri kauli ya mtu awaye yoyote kujilinda wewe na familia yako...

Unafahamu ugonjwa huu upo ndani ya mipaka ya nchi yetu, unafahamu mbinu za kupunguza nafasi ya maambukizi kwako, ukifa kwa kutokuzingatia taratibu hizi ni upumbavu wako kwa kushikiwa ufahamu na binadamu kama wewe...

Unafikiri No1 anajua nn cha ziada kuhusu Covid19 na namna ya kujikinga dhidi yake zaidi yako?? Taarifa hizi zipo kila kona
 
unachokisema ni sawa na dereva aendeshe gari mwendo wa hovyo sehemu yenye hatari kama daraja refu (lenye mamba)...halafu abiria mlio ndani mkae kimyaa mkisubiria ajali ikitokea mtamlaumu dereva!.
 
Kesho nenda mwambie Mbunge wako unachokitaka ili akiwakilshe huko Bungeni,na kitamfikia Raisi! fuata utaratibu!!
 
Kwa hiyo unaamini hiyo nafasi ya uraisi ilikua ya Lissu!?
 
Mleta mada jifunze kuficha upumbavu wako ili watu wasijue kiasi cha utapiamlo wa akili ulio nao.
Sidhani kama unajielewa, au ni ukanda unakusumbua bila kuangalia hali halisi ya nchi ilivyo!
 
Kelele za humu za makopo ya chadrama haziwezi kumzuia rais kutekeleza majukum yake mkuu
 
Hakuna aliyempa nafasi zaidi ya kutumia vyombo vya dola kupora na kufanya uharamia katika nchi!
Alipora nini? Kama 16% aliyopata Lisu haikumpa nafasi ndio unataka kuwaweka kwenye kapu moja watz wote kwamba ni bavicha hivyo hawakumpa kura Magufuli?
 
Magufuli kama anajua chanjo na mabarakoa yanaondoa kabisa corona anaanzaje kuyazuia tena itamnufaisha nini yeye kukataa chanjo we jiulize usikurupuke tu kujidai unajali Watanzania kuliko rais na serikali.
Kuna uwezekano kuwa kilichopo kwa sasa siyo Corona. Kipindi cha Corona shule zote na vyuo vyote tulifunga. Muda huu shule zote na vyuo vyote vimefunguliwa na hatujasikia hata mwanafunzi mmoja akipoteza maisha, na siombei hilo, kitu ambacho siyo rahisi kama kilichopo ingekuwa kweli ni Corona. Kuna liugonjwa fulani jingine limeibuka ambalo siyo Corona, na linatafuta watu hasa ambao wana mamlaka makubwa na wanaojulikana, ili ikitokea wamepoteza maisha, watanzania wote wasikie na pia wajue kwa sababu wengi wao wanajulikana almost na kila mtanzania. Ugonjwa uliopo kwa sasa inaonyesha kama siyo Corona. Hata hivyo tuendelee kuzingatia ushauri unaotolewa na Serikali pamoja na wataalamu wa Afya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…