Tetesi: Rais Nyusi wa Msumbiji atoroka kwa helcopter kukimbia maandamano ya wizi wa kura

Tetesi: Rais Nyusi wa Msumbiji atoroka kwa helcopter kukimbia maandamano ya wizi wa kura

Cha kufanya??
Kama wananchi tupo tayari ni kulianzisha tu,
Lakini Watanzania wengi hatuna ujasiri huo kwa sababu kulianzisha kuna gharama yake,
Tujue kabisa watu wengi watapoteza maisha na wengi watajeruhiwa.
Na pia tujue siyo wote miongoni mwetu watakaofaidika na mabadiliko tunayoyatamani kwa sababu wengine hawatokuwepo duniani kutokana na machafuko yatakayotokea.
Lakini faida wataipata wataofanikiwa kubaki hai Ikiwa viongozi watakaochukua hatamu watakuwa waadilifu.
Lakini Watanzania jinsi tunavyojuana wengi wetu ni wabinafsi hatuko tayari kujitoa kwa wengine utasikia "Niandamane nikiuliwa manufaa wapate watu wengine aah hiyo haiwezekani bwana"
Lakini tukae tukijua watawala wameanza muda mrefu kujitengenezea wao binafsi na familia zao, Na wameanza kidogo kidogo na kadri siku zinavyokwenda wanazidi kukunjua makucha yao kwa kutunga sheria za kujinufaisha binafsi na kuwabebesha mzigo wananchi hivyo wananchi wanazidi kuwa na hali ngumu,Na tayari wameajiaminisha kwamba wanaweza kufanya chochote bila kupata upinzani kutoka kwa wananchi.
 
Nauliza, kwanini kuiba kura ni halari kuiba vitu vingine siyo halari Samia Suluhu Hasani Ikulu Mawasiliano Je hiki kizazi gani mnatengeneza?
TANZANIA WIZI PEKEE AMBAO UNAKUBALIKA NA KILA MMOJA SERIKALINI KUANZIA RAIS HADI BALOZI WA NYUMBA KUMI NI WIZI WA KURA. UKIWA KWENYE MAZINGIRA YA KURA , SERIKALI ITAKUHAKIKISHA ULINZI WA HALI NA MALI ZAKO ZOTE.
 
Bado zitabaki Zimbabwe, Angola, Namibia na Afrika ya Kusini. Kote ambako Tanzania ilijifanya kusaidia kuleta uhuru ccm waliwafundisha pia kuwa wezi wa kura na kudhulumu maamuzi ya wananchi kwenye nchi hizo
Sio kwamba ANC walishinda Kihalali?
 
habari hizi ni za kweli?
Kutoka Tweeter (x)......@lifeof mshamba

MaCCM yaliwapa Teknick ya kuiba kura huko Msubiji bahati Mbaya Raia wa Msubiji Wanajitambua

Sasa hivi Wanachinjana Huko'
Chama Tawala sasa kinataka Waunde Serikali ya Mseto Raia Wamegoma Wanataka Ushindi Wao.. Mambo ya Serikali ya MSETO wakaunde na CCM
Nyusi anajutia kupokea ushauri wa CCM wa namna ya kupora maamuzi ya wananchikwenye uchaguzi.

CCM baada ya kuwaua watanzania, sasa imekuwa mshirika muhimu wa mauaji ya wananchi wa Msumbiji.

CCM imefikua kuwa adui siyo tu wa Watanzania bali mpaka wananchi wa mataifa jirani, kama Msumbjiji.
 
Sio kwamba ANC walishinda Kihalali?
Wameshinda kihalali ila ushindi mwembamba. Ccm kwa sasa tumesikia ina export mbinu za wizi wa kura. Watawafundisha. Japo wazulu hawatakubali kirahisi ujinga wa ccm
 
Itakuwa hatua nzuri na itatupa hamasa na sisi watanzania kuondoa Kwa nguvu ccm madarakani.maana Kila uchaguzi wanaipa kura
 
Na Namibia nako SWAPO hali si shwari kabisa.

Vyama kongwe dola katika mtihani mzito nchi za SADC


Matokeo yanasubiriwa huku Swapo ikikabiliwa na upinzani mkali


View: https://m.youtube.com/watch?v=BUU8qrH6eFE
Upigaji kura sasa umekamilika katika uchaguzi wa rais na wabunge wa nchini Namibia, huku Tume ya Uchaguzi ikitarajiwa kutangaza matokeo mara tu mchakato wa kuhesabu kura utakapokamilika.


Uchaguzi huu unaonekana kuwa wenye ushindani mkubwa katika historia ya hivi karibuni kwa chama tawala kongwe cha SWAPO, ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka 34.

Iwapo SWAPO itashinda, kiongozi wake Netumbo Nandi-Ndaitwah atakuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo.


Kupoteza kwa SWAPO kungeashiria uhamisho wa kwanza wa mamlaka kwa chama kipya tangu Namibia ilipopata uhuru kutoka kwa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini mwaka 1990.

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Umma Graham Hopwood anatoa maoni yake juu ya umuhimu wa uchaguzi.
 
FRELIMO ni chama kilicholelewa na TANU baadae CCM.

Wapiganaji wa FRELIMO waliishi mafichoni Tanzania.

Mipango yote ya kupambana na wareno ilifanywa na FRELIMO Tanzania.

FRELIMO imeiga yote yaliyofunzwa na chama mama [ CCM] ikiwemo mbinu za kuiba kura na kukandamiza demokrasia.

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
 
habari hizi ni za kweli?
Kutoka Tweeter (x)......@lifeof mshamba

MaCCM yaliwapa Teknick ya kuiba kura huko Msubiji bahati Mbaya Raia wa Msubiji Wanajitambua

Sasa hivi Wanachinjana Huko'
Chama Tawala sasa kinataka Waunde Serikali ya Mseto Raia Wamegoma Wanataka Ushindi Wao.. Mambo ya Serikali ya MSETO wakaunde na CCM
Thibitisha.
 
habari hizi ni za kweli?
Kutoka Tweeter (x)......@lifeof mshamba

MaCCM yaliwapa Teknick ya kuiba kura huko Msubiji bahati Mbaya Raia wa Msubiji Wanajitambua

Sasa hivi Wanachinjana Huko'
Chama Tawala sasa kinataka Waunde Serikali ya Mseto Raia Wamegoma Wanataka Ushindi Wao.. Mambo ya Serikali ya MSETO wakaunde na CCM
Hii inakuja Tz mwaka kesho. Maandalizi yameanza kufanyika jana
 
Bado zitabaki Zimbabwe, Angola, Namibia na Afrika ya Kusini. Kote ambako Tanzania ilijifanya kusaidia kuleta uhuru ccm waliwafundisha pia kuwa wezi wa kura na kudhulumu maamuzi ya wananchi kwenye nchi hizo
FRELIMO wamekuwa wakishindwa chaguzi nyingi sana, huwa wanabaki madarakani kwa figisu.
NB: Ofisi nyingi za FRELIMO zina picha za Samora na Nyerere. Birds of the same feathers flock together.
 
Vyama kongwe dola katika mtihani mzito nchi za SADC
Za ndani kwa kina :

Namibia yaongeza muda wa kupiga kura baada ya masuala ya vifaa​

10:17 | 28 Nov 2024
0 Maoni Chapisha Shiriki
Namibia kura.afp_

Maafisa wa Tume ya Uchaguzi ya Namibia wanajiandaa kuhesabu kura [Picha: Simon Maina/AFP]


Wananchi wa Namibia walikuwa bado wanapiga kura mapema Alhamisi, saa chache baada ya kura kupangwa kufungwa katika uchaguzi wa rais na wabunge uliopangwa kujaribu kushikilia madaraka kwa miaka 34 kwa chama tawala katika taifa hilo la kusini mwa Afrika.


Masuala ya vifaa yaliacha umati ukingoja kupiga kura ingawa kura zilipangwa kufungwa saa 09:00 jioni (1900 GMT) siku ya Jumatano.


Shughuli ya kuhesabu kura ilikuwa imeanza katika baadhi ya vituo huku matokeo ya awali yakitarajiwa kufikia Jumamosi kulingana na kalenda ya uchaguzi.


Katika kukabiliana na ukosoaji kutoka kwa vyama vya siasa na wapiga kura kwenye foleni ndefu, Tume ya Uchaguzi ya Namibia (ECN) ilisema inaongeza muda wa kupiga kura.
Siku ya Alhamisi asubuhi, "baadhi ya watu walikuwa bado wanapiga kura," msemaji wa ECN Siluka De Wet aliiambia AFP.


Katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia huko Windhoek, upigaji kura ulisitishwa saa 05:00 asubuhi siku ya Alhamisi, maafisa wa upigaji kura waliiambia AFP.


Kura hiyo inaweza kumletea kiongozi mwanamke wa kwanza wa taifa hilo la jangwani hata kama chama chake, chama tawala cha Afrika Kusini Magharibi cha People's Organization (SWAPO) kinakabiliwa na changamoto kubwa zaidi ya utawala wake katika siasa tangu Namibia ilipopata uhuru wake kutoka Afrika Kusini mwaka 1990.


Baada ya kupiga kura yake, mgombea wa SWAPO na makamu wa rais wa sasa, Netumbo Nandi-Ndaitwah, alitoa wito kwa watu milioni 1.5 wa nchi hiyo waliojiandikisha kupiga kura "kujitokeza kwa wingi".


'Inasikitisha kabisa'
Kulingana na sheria ya uchaguzi ya Namibia, wale walio katika foleni kabla ya uchaguzi kufungwa wanapaswa kuruhusiwa kupiga kura.
Baadhi ya wapiga kura waliiambia AFP walipanga foleni kwa saa 12, wakilaumu matatizo ya kiufundi, ikiwa ni pamoja na masuala ya tepe za kuwatambulisha wapigakura na karatasi zisizotosha za kupigia kura.


"Inasikitisha kabisa," alisema Reagan Cooper, mkulima mwenye umri wa miaka 43 miongoni mwa wapiga kura mia moja au zaidi nje ya kituo cha kupigia kura cha mji wa Windhoek.
"Wapiga kura wamejitokeza, lakini tume ya uchaguzi imetushinda," Cooper aliiambia AFP.


Wakiwa na viti vya kukunja na miavuli ili kukabiliana na mistari inayosonga polepole na jua kali, wananchi wengi wa Namibia walitumia nusu ya siku wakisubiri kupiga kura.


Wasimamizi wa tovuti ya kupigia kura waliiambia AFP kuwa matatizo ya kompyuta ya mkononi yanayotumika kukagua utambulisho wa wapigakura kwa kutumia alama za vidole ni pamoja na masasisho ya wakati, joto kupita kiasi na betri zilizokufa.


Chama kikuu cha upinzani, Independent Patriots for Change (IPC), kililaumu ECN kwa misururu mirefu na kililia mchezo mchafu.
"Tuna sababu ya kuamini kwamba ECN inakandamiza wapiga kura kwa makusudi na kwa makusudi kujaribu kuwakatisha tamaa wapiga kura kutopiga kura," alisema Christine Aochamus wa IPC.


SWAPO imetawala tangu ilipoongoza Namibia yenye utajiri wa madini kupata uhuru lakini malalamiko kuhusu ukosefu wa ajira na kuvumilia ukosefu wa usawa yanaweza kulazimisha Nandi-Ndaitwah kuingia katika duru ya pili.


Kiongozi wa IPC Panduleni Itula, daktari wa meno na mwanasheria wa zamani, alisema Jumatano alikuwa na matumaini kwamba angeweza "kuondoa vuguvugu la mapinduzi".


Kwa mara ya kwanza katika historia ya hivi karibuni ya Namibia, wachambuzi wanasema duru ya pili ya upigaji kura ni chaguo halisi.
Hilo lingefanyika ndani ya siku 60 baada ya kutangazwa kwa duru ya kwanza ya matokeo ifikapo Jumamosi.


Namibia ni muuzaji mkuu wa uranium na almasi nje ya nchi lakini sio watu wake wengi karibu milioni tatu wamefaidika na utajiri huo.
"Kuna shughuli nyingi za uchimbaji madini zinazoendelea nchini, lakini hazibadilishi katika kuboresha miundombinu, nafasi za kazi," alisema mchambuzi huru wa kisiasa Marisa Lourenco, aliyeko Johannesburg.


"Hapo ndipo huzuni nyingi zinatoka, (hasa) vijana," alisema. Ukosefu wa ajira kati ya vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 34 unakadiriwa kuwa asilimia 46, kulingana na takwimu za hivi karibuni kutoka 2018, karibu mara tatu ya wastani wa kitaifa.
Chanzo: AFP
 
Back
Top Bottom