Rais Putin aamuru kikosi maalum cha Nyuklia kuwa katika tahadhari maalum "kiwango cha juu cha tahadhari"

Mimi nijjuavyo maagizo hayo ni kuwaweka tayari Ili atakayeingilia Huo mgogoro basi ndio ziwe deployed!
Wala maandalizi ya hizo nuclear sio Kwa ajili ya kuipiga Ukraine Bali nchi yeyote itakayoingilia mgogoro Huo!
So hizo taarifa za kuwa Russia anaandaa nuclear baada ya kushindwa na Ukraine sijui mnazitoa wapi!
 
Ni intelligence failures, siku hizi majeshi ni very last option. I believe hii vita Russia angeweza kushinda kijasusi tu.
 
Wewe upo Tanzania unajuaje hajamsikiliza watu wake?
Unafuatilia habari lakini? Aliposhauriwa diplomacy akamquestion kama anapinga decision ya uvamizi jamaa akajibu kwa kubabaika sana then akamwambia nenda kakae mpaka aibu.
 
Putini mwehu tu, hapo kwenye ahadiyake ya kuwachakaza watakao msaidia Ukraine sijui anajiskiaje saizi watu wanavyo peleke misaada waziwazi na hafanyi chochote.
 
Usiongee kishabiki Putin hajashindwa vita ila alishaonya ya kuwa atakae isaidia Ukraine atajuta sasa huyu mtu atishii anamaanisha huyu wanachokosea ulaya ni kutangaza kuwa tumetoa silaha mara wanajeshi sasa Putin anakwenda kufanya unyama mkubwa mno.
Sasa mimi na wewe nani anaongea kishabiki?

Anaenda kufanya unyama mkubwa wapi, kwenye mataifa ya ulaya?
Anaenda kufanya unyama mkubwa mno kwenye aridhi ya Ukraine? Hivi nchi unayotaka kuitawala utaiteketeza kwa nyuklia si utachekwa hadi na watoto wadogo?

Unajua magnitude ya vikwazo alivyowekewa? Uchumi wake unategemea auze gesi ulaya, amepigwa pini, benki zote za Urusi hazitaopareti ulaya na marekani na pesa zilizoko huko zimesizishwa, Urusi ametupwa nje kabisa ya uchumi wa dunia!

Unajua madhara yake, Urusi lazima ashuke kiuchumi, watu wenye akili wametulia pembeni wanapiga hela kwa kuuza silaha Ukraine!

Je, hii vita ilikuwa ni a must go kwa Urusi? Sio kweli, hata kama Ukraine ingejiunga NATO bado isingeweza kuivamia Urusi na kwa hivyo isingekuwa tishio..

Kilichomfanya Putin avamie ni kuvimba kichwa kuliko pitiliza na kudhani kuwa ameshakuwa mbabe sana, kumbe...., KIBURI KINGI MBELE GIZA!

Sasa yeye si ana jeshi lenye nguvu? Sasa siku nne tu unatishia nyuklia kivipi? Au jeshi lake nguvu zake zinategemea nyuklia? Au hiyo nyuklia wenzie hawana? Jibu ni moja tu... amegundua gemu haiko rahisi kama alivyodhani ndiyo maana amekuwa wa kwanza kuomba mazungumzo..

Kuna mengi ya kuongea kuhusu Putin, lakini itoshe tu kusema ni dikteta mjinga, na nchi za magharibi wanatamani aendeleze hii vita maana inaenda kumteketeza, hiyo ni SELF SUICIDE kwa Putin!
Hata kuivamia Ukraine mliita mikwara,now Ukraine inachakaa.Soon itakuwa majivu.

Putin now hachek na mus*nge.
 
Atakamatwa Kama Kuku Timing Zinaendelea Na Atapitia Ya Sadam,Gaddafi
Nilipomsikiliza Joe Biden, moja kwa moja nilijua Putin anaenda kuwekwa mtu kati.

Kitendo cha kukanusha kwamba hawapeleki majeshi, maana yake ni kwamba wanapeleka. Kwenye THE ART OF WAR Sun Tzu anasema the whole affair of war is based on DECEIPTION, pale unapoenda, mdanganye adui kwamba huendi, ili ajisahau ukamminye.

Hawa jamaa Putin wanampiga kisayansi, wanaziga hawako na Ukraine lakini wanaisaidia kisirisiri..

Ujerumani walijisahau jana wakatamka wazi, wakasema " kupeleka kofia ngumu elfu tano pekee haitoshi, sasa wameamua bila kusita, wanapeleka 'base' ya silaha Ukrane"

Aliposema kofia ngumu elfu tano, mimi najua anamaanisha wanajeshi elfu tano... Hao ni kutoka Ujerumani peke yake.
 
Mh, hivi kama Ukraine tu imekuwa tatizo hivi anaweza kuangamiza Marekani pamoja na mataifa ya ulaya huyu Putin? I dought it, hata hivyo tuachane na Putin, mimi namuona kama dikteta aliyelewa madaraka.

Hebu nifafanulie China akiwa super power Afrika tunapigaje maendeleo kiuchumi?
 
Watu wa putin wanaoishi tz nimegundua kuwa ni wabishi ,hawaelewi,hawana fact wenyewe wanacho jua ni Russia itashinda tu itashindaje ...? Jibu Lao watalipua nuclear [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] watalipua wapi ...? Na la size gani hayo hawajui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…