Rais Putin aamuru kikosi maalum cha Nyuklia kuwa katika tahadhari maalum "kiwango cha juu cha tahadhari"

Rais Putin aamuru kikosi maalum cha Nyuklia kuwa katika tahadhari maalum "kiwango cha juu cha tahadhari"

Sawa. He gonna pay the price.
Price ipi wakati akiangusha ICBM anaifuta kabisa Ukraine! Kiherehere mwengine nae akijitokeza atatumiwa zawadi huko huko alipo 😅
 
Ukishaona rais wa nchi awaomba raia wasiokuwa na uzoefu wowote wala mafunzo ya kivita washike bunduki (wakati nchi husika ina wanajeshi wenye mafunzo na uweledi wa vita) ujue tayari jeshi hilo la nchi limeshazidiwa nguvu tayari.

Muwe mnashirikisha ubongo kuchambua mtiririko wa mambo
Sasa mbona hawaja surrender na kumuachia msala huyo Rais wao?
 
Kwani kabla ya vita si kulikuwa na mazungumzo? Si yeye ndiye aliyeacha mazungumzo na kufanya uvamizi?
Kwamba Putin ni mwendawazimu aache mazungumzo waliokubaliana kisha aanze uvamizi!

Acha uchochezi wewe Ukraine walikuwa na mkataba kuwa asijiunge na NATO wala kuhifadhi silaha zake, Ukraaine akakiuka mikataba
 
Hivi Mkuu upo dunia ya wapi wewe? Maana waonekana hujui hata habari zinazotrend ulimwenguni.

Rais wa Ukraine alikubali masharti ya Urusi ikiwemo la kuifanya Ukraine kutojiunga na NATO, wakasema wao Ukraine wanataka tu amani (link ya habari hiyo toka chanzo cha habari cha Israel ipo hapo chini).

Halafu wewe baada ya kushiba chapati za mayai kwa maharage ya kukata ya nazi na maziwa, waleta stori kuwa Ukraine kakataa masharti. Unajua vita wewe? Vita vipiganwe kwenye ardhi ya nchi yako? Tena na nchi ambayo ni super powe?

We jamaa acha kamba, msimamo wa Ukraine ni huu hapa, tena wanasema hao RT wenyewe
Screenshot_20220227-202441.png
 
Kwamba Putin ni mwendawazimu aache mazungumzo waliokubaliana kisha aanze uvamizi!

Acha uchochezi wewe Ukraine walikuwa na mkataba kuwa asijiunge na NATO wala kuhifadhi silaha zake, Ukraaine akakiuka mikataba
Na sasa baada ya 'kupigwa' kakubali kuwa hatajiunga na NATO?
 
Wewe utakuwa mzito sana kuelewa, hebu soma hapa (kama kingereza chapanda lakini)
We jamaa bana unatoa ma link ya site za wapi sijui, na kama mazungumzo hata hayajaanza tayari commitment ya Ukraine kutojiunga NATO ishatolewa au ni moja ya mambo yanayoenda kujadiliwa.?
 
Acha uzushi. Ukraine walishupaza shingo kuwa watajiunga NATO

Pia wakatiwa upepo na NATO kuwa Ukraine itapewa fursa hiyo (NATO wakijaribu kumchokonoa Putin)

Ila sasa hivi wamefunzwa na Putin kwa lugha ngumu, wamekubali kutojiunga.

Duh.. Wameshakubali tayari.?
 
Kwamba Putin ni mwendawazimu aache mazungumzo waliokubaliana kisha aanze uvamizi!

Acha uchochezi wewe Ukraine walikuwa na mkataba kuwa asijiunge na NATO wala kuhifadhi silaha zake, Ukraaine akakiuka mikataba
Acha ujinga wewe mchambuzi uchwara wa madale
 
Price ipi wakati akiangusha ICBM anaifuta kabisa Ukraine! Kiherehere mwengine nae akijitokeza atatumiwa zawadi huko huko alipo [emoji28]
Kwahy hyo ICBM anayo yeye peke ake,mwaka 1945 USA ilimufanya nn Mjapan? Halafu leo USA asiwe na huo uwezo,ficha umbumbu wako.
 
Adhibitiwe huyu mtu mbona anataka balaa kubwa kuliko!! Hii haitoshi anataka kikosi cha sumu nacho kifunguke mwemweeee, Mungu aepushie mwali kwakweli
 
Ukishaona rais wa nchi awaomba raia wasiokuwa na uzoefu wowote wala mafunzo ya kivita washike bunduki (wakati nchi husika ina wanajeshi wenye mafunzo na uweledi wa vita) ujue tayari jeshi hilo la nchi limeshazidiwa nguvu tayari.

Muwe mnashirikisha ubongo kuchambua mtiririko wa mambo
Pambana na Israel ndipo kuwa ulinzi ni jukumu la raia wote, siyo jeshi tu. Hata Tanzania baada ya kuvamiwa na Amin, JWTZ ilipanda kutoka askari 40,000 hadi kufikia laki moja na nusu. Unadhani waliiongezeka walitoka wapi kama siyo raia tu. Ukali wa jeshi kivita hutegemea uwezo wa makamanda siyo idadi ya wapiganaji.
 
R
Ukishaona rais wa nchi awaomba raia wasiokuwa na uzoefu wowote wala mafunzo ya kivita washike bunduki (wakati nchi husika ina wanajeshi wenye mafunzo na uweledi wa vita) ujue tayari jeshi hilo la nchi limeshazidiwa nguvu tayari.

Muwe mnashirikisha ubongo kuchambua mtiririko wa mambo
Raia wa ukrain, taiwan, south korea israizaeli wana pitia mafunzo ya jeshi wakiwa wanaenda college, izo uzi, M16 wana zijua
 
Back
Top Bottom