Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Sielewi una uhusiano gani na Putin kiasi cha kumtetea hivyo bila hata kutumia akili. Yaani unaamini Putin alitoa ofa ya kufanya mazungumuzo ya amani baada ya yeye mwenyewe kuwa ameshavamia na kuvunja amani hiyo? Hivi wewe unajua sababu ya Putin kuivamia Ukraine? Uvamizi huu umesababisha Ukraine itajiunga na NATO haraka sana; ilikuwa inacheleweshwa na sababu za rushwa, na Putin amechukia sana kwa rais wa sasa wa Ukraine kusifiwa kwa kukomesha rushwa, ambayo ndiyo ilikuwa kikwazo kikubwa. Unaona sasa hivi Sweden na Norway nazo zinajiunga na NATO, eti nazo anazitishia. Huyu jamaa kapungukiwa sana akili.Putin alitoa Offer ya mazungumzo toka ijumaa tena kwa masharti. Na Ukraine ikakubali masharti hayo. Angekuwa na uwezo angekubali masharti hayo? Mbona kabla ya kuchapwa alikuwa akishupaza shingo kuwa watajiunga NATO lakini baada ya kuchapwa kakubali kutojiunga?
![]()
Mtu akikaa madarakani muda mrefu tena kwa mabavu, huwa hapati habari sahihi nje ya anavyotaka kusikia, na hilo ndilo tatizo lake. hata kwenye ule mkutano wako na wana usalama wake walikuwa wakitaka kumpinga ila wakamkubalia kwa shingo upande kwa vile hilo ndilo alilokuwa anataka kuskia, na limekuwa ni kosa kubwa sana.