Rais Putin aamuru kikosi maalum cha Nyuklia kuwa katika tahadhari maalum "kiwango cha juu cha tahadhari"

Hata kuishambulia Ukraine mlisema ni mikwara tu na amefanya kweli, sidhani kama Russia itakubali kushindwa hii vita wakati ina silaha za maangamizi bora wakose wote, ndio kinachoenda kutokea, waangamizane kisha China iinuke kuwa super power, labda na sisi huku Afrika tutaweza kupiga hatua ya maendeleo kidogo
 
Wewe unaongelea taarifa ya asubuhi. Huyo comedian kaufyata na anaenda Belarus kwa mshirika wa Russia.

Acha uongo, imekubalika wakutane mpakani wote kwenye mazungumzo. Amegoma kwenda Belarus Kama proposal ya Russia ilivyotaka. Nimekubali Sana Rais wa Ukraines kwa uzalendo wake , hakukimbia nchi Bali ameenda uwanja wa Vita na kukataa proposal ya Putin. Mpaka kupelekea mpakani Yani neutral ground. Yule jamaa hamuogopi Putin.
 

Vita vinapiganiwa jirani na Russia. Nani akose Tena. Russia ndio atapoteza zaidi kuliko Ukraine maana Ni majirani. Kwanza Ukraine ndio ataingia Nato na EU baada ya kuona Russia Ni adui yake.
 
Ameshapaniki baada ya nchi za Magharibi kujua mbinu zake na tegemeo lake ndo hizo nyuklia, ambazo mataifa makubwa ya magharibi wanazo
 
Hata warusi wa mbagala wanamdharau sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…