HERY HERNHO
Senior Member
- Mar 4, 2022
- 110
- 458
Hotuba ya mwaka ya Putin yatowa mwelekeo wa Urusi kuhusu vita nchini Ukraine wakati rais wa Marekani Joe Biden akitarajiwa kuwahutubia washirika wake akiwa Poland baada ya kuitembelea Kiev Jumatatu.
Hotuba ya Putin kwenye bunge la nchi hiyo imetowa tathmini kwa viongozi wa kisiasa na kijeshi kuhusu vita vya Ukraine lakini pia tathmini ya hali ilivyo kimataifa pamoja na kutowa mwelekeo wa hali halisi ya nchi hiyo baada ya nchi za Magharibi kuiwekea vikwazo chungunzima.
Rais Vladmir Putin amesema nchi za Magharibi bado zinaendelea kumimina fedha kuunga mkono vita na nchi hizo zilianza kuifanya Ukraine kuwa mpinzani wa Urusi muda mrefu. Na kwa hivyo amekwenda mbali zaidi kwa kusema nchi hizo zinawajibika kubeba dhamana kikamilifu juu ya vita hivyo. naambatanisha na link hii sikia alichosema
Mara chungunzima Rais huyo wa Urusi amekuwa akitowa sababu za kuhalalisha uvamizi wake nchini Ukraine kwa kuzituhumu nchi za Magharibi kwamba zinaitishia nchi yake. Hii leo pia amerudia hayo hayo akisisitiza kwamba nchi za Magharibi ndizo zilizoanzisha vita hii na Urusi inatumia nguvu kuimaliza vita hiyo na inapambana kurudisha haki ya kihistoria.