Victorie nakupendaga sana dada yangu.
Lakini Putin ama Russia wala sio wapenda vita kama USA.
Unajua USA anatamani sana kuizunguka Urusi kwa kuweka silaha zake?
Je Urusi anyamaze TU.
Unajua sula la ulinzi na usalama wa nchi ndio ajenda namba moja ya nchi yoyote?
Unafahamu huyuhuyu Marekani aliwahi kupelela makombora ya nyukilia Uturuki ili kumlenga Urusi ya zamani?
Unafahamu majibu ya Urusi kwa jambo hilo?
Urusi naye akapeleka silaha za nyukilia Cuba.
Unafahamu Nini kilitokea?
Ni Marekani alikubali kuondoa haraka sana nyukilia zake na Urusi ndipo nae akaondoa Nyukilia zake Cuba.
Sasa bado Marekani anatamani sana kuizunguka Urusi kijeshi,na Urusi hakubali.
Ndio sokomoko lote hilo.
Hebu fikiria Marekani Yuko ma maili na ma kilometa mbali kabisa huko Huku ulaya anatafuta Nini na NATO yake?
Yeye hakai ulaya NATO ya Nini?
Urusi anapenda kuishi kwa amani sana na Europe ili wafanye biashara,awauzie gesi na mbogamboga na mafuta,nae anunue vitu kwao.USA hapendi Hali hii.
USA hapendi mradi wa Bomba la gesi kutoka Urusi kwenda Ujerumani na ulaya.anajua Urusi itafanikiwa sana kiuchumi ndio Kaanzisha fitina hizi ili kumzuia .na baadae aje kuwaambia euro wamuwekee vikwazo ili kumlostisha.
Urusi anapenda kufanya biashara na kushirukiana na Ulaya, Marekani hapendi Hali hii ndio anawachonganisha,anaforce kujiunga Ukraine katika NATO.
Pia Ukraine kujiunga na NATO ni hatari kwa usalama wa Urusi,kwani itakua rahisi kuichunguza Urusi na hata ikitokea vita huko mbeleni inakua rahisi kwa UsA na NATO kuivamia ama kuishambulia Urusi.
Urusi wanalijua hilo,na wako tayari kupoteza uchumi lakini walindw taifa lao kwa gharama yoyote ile.na ndio unaona haya Leo hii.
Urusi ni taifa la kiungwana sana na Putin sio mtu katili.
Kuhusu kufunga wapinzani wake,hayo Sasa Mimi siwezi kuyaelezea kwa sababu hizo ni siasa za ndani sijui chochote inawezekana kweli wanamakosa ama anawaonea TU.sijui kitu.