Rais Ruto wa Kenya amewakaribisha na kuwaahidi kuwapa wafanyakazi million moja Saudi Arabia, kinyume kabisa na Tanzania

Rais Ruto wa Kenya amewakaribisha na kuwaahidi kuwapa wafanyakazi million moja Saudi Arabia, kinyume kabisa na Tanzania

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Licha ya maandamano yanayoendelea Kenya, Rais Ruto amewakaribisha Saudi Arabia wawekeze wapendavyo na amewataka waitumie fursa ya kufunguwa viwanda kwani Kenya ina mikataba ya misamaha ya kodi ya bidhaa zake nchi za Ulaya.

Pia amewaahidi atawapa wafanyakazi million moja ndani ya muda mfupi, hivi sasa Kenya ina wafanyakazi laki mbili Saudi Arabia.

Katika maongezi hayo, Sai Arabia imewaahidi Kenya kuwapa mafuta ya gharama nafuu ndani ya miezi miwili ili kuwapunguzia tatizo la mfumko wa bei linalowakabili Kenya sasa hivi.

Sasa naelewa kwanini Kenya haina maliasili za kutosha lakini imetupita sana kiuchumi. Wana fikra za kimaendeleo, kinyume na sisi tuna fikra za kichawi za kurudishana nyuma tu.

Ushahidi huu hapa:

 
Katika kuelezea kwako sakata la Dubai na uwekezaji hapa nchini naona unaandika kwa haraka na kukosa umakini wa uandishi kila unapo andika.
Kenya unaita Kenye nk.

Naona wewe ni mhusika Mkuu wa karibu kabisa wa huu uwekezaji unaoupigia chapuo kwa jasho na damu.

Sisi hatuukatai mkataba wala Waarabu, tunakataa vipengele vyake tu. Rekebishani tu mfanye nao biashara bila wasi wasi.
 
Kuna kitu unalazimisha wakati sio halisi na kweli.

Hakuna nchi inayokataa wawekezaji wa kigeni, hata Tanzania tunataka sana waarabu wawekeze Tanzania, lakini hakuna nchi inayotaka wawekezaji wa kigeni waje kumilikishwa rasilimali zao ili wananchi wao wabakie watumwa na manamba wa wageni, hata Tanzania hatutaki huo ujinga.

Yote kwa yote, machafuko ya kila mara ya Kenya hayawezi kumvutia muwekezaji yoyote.
 
Naona wewe ni mhusika Mkuu wa karibu kabisa wa huu uwekezaji unaoupigia chapuo kwa jasho na damu.
Mimi natamani sana DP World waanze kazi leo kabla ya kesho. Nafahamu faida zake. Namshuru Mwenyezi Mungu nilipata "exposure" kubwa sana duniani huko.

Naifahamu Dubai na jinsi wanavyofanya biashara zao kiuaminifu mkubwa sana.

Waulize wafanya biashara na wajasiriamali tu wanaofanya kazi zao na Dubai. Watakueleza.
 
😄😄 Mlokole Ruto anainyoosha Kenya kama Shujaa Magufuli

Mlokole Gachagua: Tumeweka mitego kila kona Wananchi pigeni kazi Yesu anaokoa

Kenya wanajitambua sana 🤣🤣
Sana, likija suala la uchumi Kenya hatuwapati kabisa. Wapo mbali sana na wakati sisi tunalumbana kijinga huku Waarabu na vigati vya bandarini, wao wanawatafuta Waarabu na wanawaambia njooni muwekeze mnachotaka hapa.
 
Licha ya maandamano yanayoendelea Kenya, Rais Ruto amewakaribisha Saudi Arabia..

Hakuna mtu anayekataa wawekezaji. Tatizo mmeuhamisha mjadala kutoka kwenye aina ya mkataba hadi kwenye kukataa muwekezaji n.k.

Hii inaonyesha tunaoukataa Mkataba huu tuna hoja ndiyo maana mmejikuta mmehamisha magoli ili na nyie mfunge.

Ipo hivi;
Kuwekeza Vs kumilikishwa.
Mikataba yenye tija Vs Mikataba ya kimangungo.
 
Mimi natamani sana DP World waanze kazi leo kabla ya kesho. Nafahamu faida zake. Namshuru Mwenyezi Mungu nilipata "exposure" kubwa sana duniani huko.

Naifahamu Dubai na jinsi wanavyofanya biashara zao kiuaminifu mkubwa sana.

Waulize wafanya biashara na wajasiriamali tu wanaofanya kazi zao na Dubai. Watakueleza.
Nimekuandikia hapo juu. Naona hata kusoma hutaki.
Ngoja nikuwekee tena hapa.

"Mambo kama ya Tanzania will inform Dubai in all other ports opportunities including Lakes hatuyataki.
Tanzania ni nchi huru na kubwa kupita UAE, hiyo minyororo haitakubalika.
Na hayo mengine unayajua"

Hizo haraka zenu tunaweza kuziita ni UKUWADI haramu.
Nini kinawashinda kuwasikiliza wenye nchi ?
Haraka ya kuwasujudia Waarabu unayotaka sio.
 
Back
Top Bottom