Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

 

Attachments

  • 76C2B670-54B8-470B-B4F1-8C8189D552D1.jpeg
    76.1 KB · Views: 1

 
Swali langu daima limekuwa hili "Je wale wote waliofundishwa na wanaodaiwa kuwa na vyeti feki wakafaulu mitihani na wengine wana PHD wengine maofisa wakubwa nao waadhibiwe kama waalimu wao?" Mbona tunaangalia upande hasi pekee kwa nini hatuangalii na upande chanya pia kisha tukayapima na kutoa hukumu stahiki? Kuna watu walijiendeleza, wakafaulu mitihani, wakabobea katika fani zao, lakini kwa sababu ya jina tu wakapoteza haki zao bila kuangalia mazuri waliyoyafanya. Hiyo ni haki kweli?? Jamani angalieni na upande wa pili, msiwaumize kwa kuwa tu nyie mnadhani mko salama katika nafasi zenu. Maisha ni safari ndefu.
 
Hizi ni juhudi za kuendelea kumgombanisha Rais na wananchi. Hii ni mpango mahsusi ikiratibiwa na kijana wake mpenzi alie mpa wizara ya fedha akishirikiana kwa karibu sana na Sukuma gang ili Mama afeli yeye awe Rais.
Hakuna agizo Mama amewahi kutoa linalo husu pesa lijatekelezwa na Mwigulu. Nasema Mwigulu ndie mchonganishi wa Rais na wananchi. Days will tell..
 
Wewe ndiye wa hovyo!

Hujui hata unachopigia kelele!

Una roho ya korosho ya dhuluma.
 
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Hatuwezi kufanya haramu kuwa haki huu utakuwa uwenda wazimu wa mchana kweupe kila mtu lazima alipwe kwa matendo yake walio na vyeti fake acha wavune walicho panda.

"Dira ya taifa ni moyo wa taifa"
 
Wakati wanaghushi vyeti hawakujua kuwa ni kosa kisheria. Unapoleta huruma zisizo na msingi katika vitu sensitive kama elimu unakosea sana mkuu.

Zamani sisi tulikuwa tunarudia darasa baada ya kufeli shule, kwa nini wao wakaamua kutumia shortcut ya kununua vyeti vya ndugu zao badala ya kurudia madarasa na mitihani?

Ukitetea ujinga kisa huruma ndio tunaishia kuwa taifa pa hovyo kabisa.
 
Watalipwa na hilo halina ubishi sasa sijui wewe linakuuma nini.
Kama una upeo mdogo utasema hawalipwi.

Ila utaratibu wa kulipwa upo palepale kama taratibu zimefatwa kama ilivyoelekezwa.
Uchambuzi unafanyika ili kusiwe na hasara either kwa mfanyakazi au mifuko kumbuka kuna walokua wanachangia 10% na wengine 5% kulingana na mikataba ya ajira zao.
Hawawezi kulipa malipo feki kwa wafanyakazi walokuwa na vyeti feki.
 
Yaaani mtu amefanaya kosa la jinai anaambiwa alidhurumiwa!
Je wale waliokuwa majumbani na vyeti vyao halisi wao walisoma bure et.
Mtu asote kusoma tena kwa shida halafu atokee mtu hana shule aajiliwe kweli!
Tena ningekuwa mimi ndiye rais ningesweka ndani wote.
Mbaaafuuuu.
 
Wakati ukishabikia, wenye akili tulikuonya ila kutokana na kibri chako cha uandishi wa habari na uchadema wako mbuzi, ukatuona juha
 
Actually wamerudishiwa/wameanza kurudishiwa michango yao. Ninamfahamu mmoja kalipwa. Alikuwa Mwalimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…