Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Jaman kuna wenye vyeti halali pia wako mitaani miaka mitano after chuo mpaka wengine sita wanajiita mashangazi then mnakuja bado mnashuhulika na waliokuwa wameidanganya serikali na wakalipwa salaries. Tuwe fair. Hao ninaowasemea wanajisikiaje wakisikia walionunua vyeti bado wanalipwa mafao..?
 
Wadau wenzangu,awali ya yote naomba nijitokeze pasipo uoga na kwa ujasiri kumpongeza Raisi wetu mpendwa Mama Samia kwa juhudi zako za kuiendesha nchi na kufanikisha yale yote mliyoanzisha wewe na mtangulizi wako Marehemu Magufuli pia kuleta mapya ya kuhakikisha wananchi wako tunafurahia matunda ya kodi zetu bila kutapanya misaada na mikopo tuipatayo toka kwa wahisani.

Mama Samia mimi ni mhanga wa kuondolewa kazini kwa cheti feki.Naomba kwa niaba ya wenzangu nilete shukrani zetu kwako kwa kutambua mchango wetu,juhudi na bidii zetu kwenye kujenga nchi yetu,na Ukaamuru tulipwe stahiki zetu zile tulizochangia kwenye uchumi wa Tanzania yetu.

Japo hatujalipwa bado,lakini tunaendelea kuwa na imani na serikali yako kwamba siku moja tutapata haki yetu,maana kauli ya Raisi ni amri kwa watendaji wote wa serikali. Mwisho niwaombe wenzangu msione aibu kujitokeza hapa hadharani,kujibu hoja za wasioelewa kwamba si wote walioondolewa kazini kwamba walikuwa si halali.

Sitamsemea mtu,tusubiri mjadala kama mode hawataondoa andiko hili,natumaini, maswali na kejeli vyote vitajibiwa.

Ahsante
 
Nchi yenu haina ajira
 
Yaani tapeli unasema amedhulumiwa na serikali! Akili yako kama ya Mbowe tu.
 
Na walioajiri watu ambao hawana sifa wamefanywa nini?
 
Watalipwa hutaki kajinyonge
 
Utabadili ID weee lakini haisaidii.
Mama ameupiga mwingi, ni mwenye huruma na mwingi wa rehema.
Watalipwaaaaa
 
Hamkustahili hata mia,mlidhurumu haki za walio stahili hizo nafasi.
 
Siwalaumu waliofoji vyeti na kuvitumia katika nafasi mbalimbali. Dunia ya sasa what matters a lot is EXPERIENCE. Wapo watu kibao wanaendelea na majukumu maofisini kwao huku wakiwa hawana ujuzi stahiki wa like kinachopaswa kufanyika na wanaofanya. Ukiwa na supervisor mwerevu, mfoji cheti ataishi katika werevu huo huo wa senior wake.
 

Wezi wakijisifia kuhusu wizi wao

Kutwa mko humu kulalamikia ufisadi Serikalini wakati nyie ndo mafisadi wakubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…