Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Jaman kuna wenye vyeti halali pia wako mitaani miaka mitano after chuo mpaka wengine sita wanajiita mashangazi then mnakuja bado mnashuhulika na waliokuwa wameidanganya serikali na wakalipwa salaries. Tuwe fair. Hao ninaowasemea wanajisikiaje wakisikia walionunua vyeti bado wanalipwa mafao..?
 
Wadau wenzangu,awali ya yote naomba nijitokeze pasipo uoga na kwa ujasiri kumpongeza Raisi wetu mpendwa Mama Samia kwa juhudi zako za kuiendesha nchi na kufanikisha yale yote mliyoanzisha wewe na mtangulizi wako Marehemu Magufuli pia kuleta mapya ya kuhakikisha wananchi wako tunafurahia matunda ya kodi zetu bila kutapanya misaada na mikopo tuipatayo toka kwa wahisani.

Mama Samia mimi ni mhanga wa kuondolewa kazini kwa cheti feki.Naomba kwa niaba ya wenzangu nilete shukrani zetu kwako kwa kutambua mchango wetu,juhudi na bidii zetu kwenye kujenga nchi yetu,na Ukaamuru tulipwe stahiki zetu zile tulizochangia kwenye uchumi wa Tanzania yetu.

Japo hatujalipwa bado,lakini tunaendelea kuwa na imani na serikali yako kwamba siku moja tutapata haki yetu,maana kauli ya Raisi ni amri kwa watendaji wote wa serikali. Mwisho niwaombe wenzangu msione aibu kujitokeza hapa hadharani,kujibu hoja za wasioelewa kwamba si wote walioondolewa kazini kwamba walikuwa si halali.

Sitamsemea mtu,tusubiri mjadala kama mode hawataondoa andiko hili,natumaini, maswali na kejeli vyote vitajibiwa.

Ahsante
 
Nchi yenu haina ajira
 
Na walioajiri watu ambao hawana sifa wamefanywa nini?
 
Uongozi wa serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania kuweni na aibu wakati mwingine hivi unawezaje kumlipa mtu ambaye alikuibia ? kama ni msamaha mliwasamehe kwa kuwafuta kazi maana yake ni kwamba mshahara waliokuwa wanapata kupitia ajira ya vyeti hivyo mliona unatosha na kuwafuta kazi.

iweje leo watu walioghushi vyeti na kuibia serikali walipwe pesa za umma ! Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania asifikri kulipa malipo hayo ni sifa bali atakuwa amejichafua mwenyewe hii itamaanisha hakuna umakini uliopo katika serikali anayoiongoza.

kuna tetesi kuwa yale ma vyeti ya posta kila mtu ananunua kwa wakati wake na wa nunuzi wakuu ni watu ambao walishapata ajira serikalini na hununua waliowengi ili waweze kupanda madaraja kulingana na elimu zao kwa sasa kila mtu anakula kulingana na urefu wa kamba yake.

Baada ya kuielewa ccm vyema na serikali kwakweli hata mimi nimeona nianze kujiongeza kwa baadhi ya mambo ili mradi nisije kupata tatizo lolote.
nchi hii ukijifanya mzalendo wa kila kitu utakufa masikini.

Ushahidi mkubwa nilioona ni pale mwenyekiti wa chama cha ccm na raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania ambao alianza kutukana wakosoaji wake ndani ya chama kwa kusema mtu anayejuwa itikadi za chama hawezi kuleta nongwa hii alimaanisha hataki watu wakosoe mabaya yanayofanyika ndani ya nchi hasa ukiwa ndani ya ccm, sasa ajue kuwa nchi hii siyo miliki ya ccm ataondoka ataiacha na hawezi juwa ni viongiozi gani watakuja asishangae akaitwa mahakamani kwa makosa aliyoyafanya akiwa raisi, lipa vyeti feki hiyo haifutiki siku moja utaulizwa maswali.
Watalipwa hutaki kajinyonge
 
Wadau wenzangu,awali ya yote naomba nijitokeze pasipo uoga na kwa ujasiri kumpongeza Raisi wetu mpendwa Mama Samia kwa juhudi zako za kuiendesha nchi na kufanikisha yale yote mliyoanzisha wewe na mtangulizi wako Marehemu Magufuli pia kuleta mapya ya kuhakikisha wananchi wako tunafurahia matunda ya kodi zetu bila kutapanya misaada na mikopo tuipatayo toka kwa wahisani.

Mama Samia mimi ni mhanga wa kuondolewa kazini kwa cheti feki.Naomba kwa niaba ya wenzangu nilete shukrani zetu kwako kwa kutambua mchango wetu,juhudi na bidii zetu kwenye kujenga nchi yetu,na Ukaamuru tulipwe stahiki zetu zile tulizochangia kwenye uchumi wa Tanzania yetu.

Japo hatujalipwa bado,lakini tunaendelea kuwa na imani na serikali yako kwamba siku moja tutapata haki yetu,maana kauli ya Raisi ni amri kwa watendaji wote wa serikali. Mwisho niwaombe wenzangu msione aibu kujitokeza hapa hadharani,kujibu hoja za wasioelewa kwamba si wote walioondolewa kazini kwamba walikuwa si halali.

Sitamsemea mtu,tusubiri mjadala kama mode hawataondoa andiko hili,natumaini, maswali na kejeli vyote vitajibiwa.

Ahsante
Utabadili ID weee lakini haisaidii.
Mama ameupiga mwingi, ni mwenye huruma na mwingi wa rehema.
Watalipwaaaaa
 
Hamkustahili hata mia,mlidhurumu haki za walio stahili hizo nafasi.
 
Siwalaumu waliofoji vyeti na kuvitumia katika nafasi mbalimbali. Dunia ya sasa what matters a lot is EXPERIENCE. Wapo watu kibao wanaendelea na majukumu maofisini kwao huku wakiwa hawana ujuzi stahiki wa like kinachopaswa kufanyika na wanaofanya. Ukiwa na supervisor mwerevu, mfoji cheti ataishi katika werevu huo huo wa senior wake.
 
Wadau wenzangu,awali ya yote naomba nijitokeze pasipo uoga na kwa ujasiri kumpongeza Raisi wetu mpendwa Mama Samia kwa juhudi zako za kuiendesha nchi na kufanikisha yale yote mliyoanzisha wewe na mtangulizi wako Marehemu Magufuli pia kuleta mapya ya kuhakikisha wananchi wako tunafurahia matunda ya kodi zetu bila kutapanya misaada na mikopo tuipatayo toka kwa wahisani.

Mama Samia mimi ni mhanga wa kuondolewa kazini kwa cheti feki.Naomba kwa niaba ya wenzangu nilete shukrani zetu kwako kwa kutambua mchango wetu,juhudi na bidii zetu kwenye kujenga nchi yetu,na Ukaamuru tulipwe stahiki zetu zile tulizochangia kwenye uchumi wa Tanzania yetu.

Japo hatujalipwa bado,lakini tunaendelea kuwa na imani na serikali yako kwamba siku moja tutapata haki yetu,maana kauli ya Raisi ni amri kwa watendaji wote wa serikali. Mwisho niwaombe wenzangu msione aibu kujitokeza hapa hadharani,kujibu hoja za wasioelewa kwamba si wote walioondolewa kazini kwamba walikuwa si halali.

Sitamsemea mtu,tusubiri mjadala kama mode hawataondoa andiko hili,natumaini, maswali na kejeli vyote vitajibiwa.

Ahsante

Wezi wakijisifia kuhusu wizi wao

Kutwa mko humu kulalamikia ufisadi Serikalini wakati nyie ndo mafisadi wakubwa
 
Back
Top Bottom