Wadau wenzangu,awali ya yote naomba nijitokeze pasipo uoga na kwa ujasiri kumpongeza Raisi wetu mpendwa Mama Samia kwa juhudi zako za kuiendesha nchi na kufanikisha yale yote mliyoanzisha wewe na mtangulizi wako Marehemu Magufuli pia kuleta mapya ya kuhakikisha wananchi wako tunafurahia matunda ya kodi zetu bila kutapanya misaada na mikopo tuipatayo toka kwa wahisani.
Mama Samia mimi ni mhanga wa kuondolewa kazini kwa cheti feki.Naomba kwa niaba ya wenzangu nilete shukrani zetu kwako kwa kutambua mchango wetu,juhudi na bidii zetu kwenye kujenga nchi yetu,na Ukaamuru tulipwe stahiki zetu zile tulizochangia kwenye uchumi wa Tanzania yetu.
Japo hatujalipwa bado,lakini tunaendelea kuwa na imani na serikali yako kwamba siku moja tutapata haki yetu,maana kauli ya Raisi ni amri kwa watendaji wote wa serikali. Mwisho niwaombe wenzangu msione aibu kujitokeza hapa hadharani,kujibu hoja za wasioelewa kwamba si wote walioondolewa kazini kwamba walikuwa si halali.
Sitamsemea mtu,tusubiri mjadala kama mode hawataondoa andiko hili,natumaini, maswali na kejeli vyote vitajibiwa.
Ahsante