Pre GE2025 Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nilioweka ni ya kidonge mkuu,
 
Kwa hiyo vidonge si miezi mitatu ndio inabidi uuze?
 
Nyanda za juu kusini na wakulima wote nchini wamejaa raha ,furaha na tabasamu katika Nyuso na mioyo yao.
Chakula ni bidhaa muhimu inayotumika kila siku. Je, kupanda kwake bei hiyo ni furaha au huzuni?
 
Ndio .japo unaweza ukaongeza dawa tena na kuendelea kuyatunza tu.si unaonaga wengine wanauza hadi mwezi wa kwanza yanapokuwa na bei kubwa.
Ni kweli, hofu yangu nawaza yasije liwa na wadudu tu, maana ndio mara ya kwanza naanza hizi harakati za kununua na kuweka stoo.
 
Ukiona serikali inaingilia mpaka biashara za kufanya wanainchi wa kawaida jua kibubu Kina Hari mbaya
 
Ukiona serikali inaingilia mpaka biashara za kufanya wanainchi wa kawaida jua kibubu Kina Hari mbaya
Dhamira ya serikali yetu ni kumuinua mkulima. Ndio maana inaweka bei nzuri.lakini hujalazimishwa kuuza mahindi yako serikali.uza unapotaka Mwenyewe
 
Mimi nilishawahi kuwa na mahindi, nilikuwa nauza gunia kuanzia TZS 90,000 hadi 110,000. Maana yake kg ni 900 mpaka 1100. Ni gunia la kg 100.
 
Watu wapo Dar hawajui chochote kuhusu kilimo. Aisee, nimeshangaa sana watu kufurahia bei ya TZS 700 kwa kg!
 
Mama anaupiga mwingi.
Kwani siku hivi Wakenya wameacha kununua mahindi!? Kwa uzoefu wenu ni miezi gani ambayo bei ya mahindi inakuwa juu na ni ipi inakuwa chini na kwa sababu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…