Rais wa Tanzania Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote Tanzania ikiwemo TAKUKURU Mhe Samia Suluhu Hassan amesema haya...
"Mkurugenzi wa TPA, Waziri na TAKUKURU mpo, naamrisha ripoti ya CAG mkaisome, halafu mchukue hatua, fedha nyingi sana imepotea watu tunachekeana tu, na bado waliotajwa kwenye ripoti bado wapo maofisini wanaendeleza wizi,"
==
Ukweli ni kwamba Tanzania sasa kumekucha na Rais ni Jemedari Mkuu Samia Suluhu Hassan
Moto kwa majizi yote ya fedha za umma ni rasmi sasa unawaka na siku zao zinahesabika kwa vidole.
Wale wote waliokuwa wanamchukulia " Poa Mama " sasa wakae mkao wa kunyolewa
Sasa kama ulitajwa na CAG umetafuna cha Umma kaa mguu sawa, Tutaelewana tu ngoja tuone
Ushauri wangu nyie wenye dhamana acheni kugusa pesa ya Umma huyu mama sio Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli aliyewachekea na kuangalia asiowataka tu