Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,823
- 2,466
===
Rais Samia Suluhu Hassan leo tarehe 01|05|2022 ambayo ni siku ya "Mei Mosi "
Rais wetu ametangaza neema kwa wafanyakazi wa Serikali anayoiongoza,
Mtakumbuka ni miaka sita sasa Wafanyakazi wa Serikali ya Tanzania hawakupandishwa mishahara significantly,
Tunakumbuka, Rais Samia alipokuwa Jijini Mbeya katika Mei Mosi yake ya kwanza ya 01|05|2021
Rais Samia aliwaahidi Wafanyakazi angewaongeza mishahara mwaka huu wa 2022,
Hatimaye Rais huyu anayetajwa kuwa msikivu zaidi kuwahi kutokea hapa Tanzania ameongeza mishahara kwa kiwango kitakachotolewa hapo baadae
Mtakumbuka TUCTA walipendekeza kuwa kima cha chini kiwe TZS 1,010,000,
Hongera Rais Samia, Hongera Wafanyakazi, Hongera Tanzania,Hongera CCM,
Alichosema Rais Samia;
===
“Lile jambo letu lipo. Ndugu zangu jambo letu lipo ila sio kwa kiwango kilichosemwa na TUCTA kwa sababu mnajua hali ya uchumi wa nchi yetu na hali ya uchumi wa dunia. Hali si nzuri sana uchumi wetu ulishuka chini mno. "
"Tumejitahidi sana na kwa sababu nilishatoa ahadi mwaka jana, kwa hiyo nimeagiza jambo liwepo, mahesabu yanaendelea, tutajua lipo kwa kiasi gani. Lakini jambo lipo”
===
Lazima tuelewe kutaja ongezeko la mishahara ya watu hadharani ni kuchochea mfumuko wa bei nchini,Sasa tukachape kazi kwa bidii,