Rais Samia aahirisha ziara yake ya Cuba

Rais Samia aahirisha ziara yake ya Cuba

There is something not right. Did she invite herself? The Foreign, Cultural and Health Ministers should be taken to task pamoja na private office. It's shameful.
 
Inasikitisha sana mtu una smart simu halafu unashiindwa hata kufuatilia kitu kidogo kinachoendelea Cuba. Gridi ya umeme ya taifa na viwanja vya ndege vimefungwa na hali ni mbaya bado unasema: "Watakuwa hawakujipanga" please JF ni jukwaa kubwa tuliheshimishe kwa hoja zetu.🙏🙏🙏
Asante kwa taarifa
 
TAARIFA KWA UMMA

KUAHIRISHWA KWA ZIARA YA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ILIYOKUWA IFANYIKE NCHINI CUBA

Havana, 07 Novemba, 2024

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuutaarifu umma kwamba ziara ya kitaifa ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyopangwa kufanyika tarehe 6 hadi 8 Novemba, 2024 nchini Cuba imeahirishwa.

Ziara hiyo imeahirishwa kufuatia taarifa rasmi iliyowasilishwa na Serikali ya Cuba ikitaarifu kuwa Cuba ingekumbwa na Kimbunga Rafael kuanzia tarehe 6 hadi 7 Novemba, 2024. Hali hiyo imepelekea Serikali ya Cuba kuchukua tahadhari ikiwemo kusitisha safari zote za ndege kuingia na kuondoka Cuba.

Pamoja na kuahirishwa kwa ziara hiyo, Mhe. Rais ameelekeza shughuli zote zilizopangwa kufanyika kipindi cha ziara yake ziendelee kuratibiwa chini ya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akishirikiana na Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Ziara nyingine ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Cuba itapangwa siku za usoni baada ya nchi hizo mbili kukubaliana wakati sahihi wa ziara hiyo

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

PIA SOMA
- Rais Samia kuisimamisha Dunia kutokea Cuba hapo Kesho

- Waziri Kombo aongoza kikao cha maandalizi ya ziara ya Rais Samia nchini Cuba
 
Attachments

  • 1731053871203.png
    1731053871203.png
    60.4 KB · Views: 1

Tutajua tu!
 
Sawa imekuwa muda, yuko wapi sasa mkuu wa nchi yetu au likizo USA
 
Kwani Zaidi ya Wizara ya mambo ya nje, chombo gani kingine cha habari cha Canada kilitaarifu kuhusu kutokea kwa Kimbunga Rafael tarehe 6-7?
 
Nilisikia anaenda Cuba kuudhuria kongamano la kiswahili ni upotevu wa rasilimali tu
 
RAIS SAMIA KUIBUKIA ZIMBABWE ?

SADC inapanga mkutano wa kilele usio wa kawaida wenye dharura kubwa mjini Harare – kuangalia uchaguzi wa Msumbiji, Botswana​

Na Thandiwe Garusa

Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) inatazamiwa kufanya mkutano wa dharura mjini Harare wiki ijayo, na huku uchaguzi wa hivi karibuni wa Msumbiji na Botswana na masuala mengine ya kikanda ya usalama kuwepo kwenye ajenda kuu.

Mwezi Agosti,2024 Zimbabwe ilipata heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa 44 wa SADC ambapo Rais Emmerson Mnangagwa alichukua uenyekiti wa mzunguko wa jumuiya hiyo ya kikanda.

Akihutubia wanahabari wakati wa mkutano wa baada ya baraza la mawaziri Jumanne, Waziri wa Habari wa Zimbabwe mheshimiwa Jenfan Muswere alisema mkutano huo utafanyika kuanzia Novemba 16 hadi 20, 2024
1731259851332.jpeg

Picha: waziri Jenfan Muswere

"Taifa linafahamishwa kuwa mkutano wa dhararu wa Wakuu wa Nchi na serikali wa SADC umepangwa kufanyika Harare kuanzia tarehe 16 hadi 20 Novemba 2024, hasa kushughulikia masuala ibuka ya umuhimu wa kikanda
 
View attachment 3148895

Ni jambo jema
 
Inatolewa taarifa kuwa Rais atakuwa nchi fulani kwa ziara ya kikazi. Tunapewa ratiba yenye kila kitu na ndege ya Rais inaondoka hadi kufika eneo husika. Mara ghafla tunaambiwa Rais ameahirisha ziara bila kuelezwa kisa ni nini. Lakini ndege ipo eneo la ziara.

Cha ajabu ndege inaonekana kuondoka eneo la ziara kurudi nchini bila kuwa na taarifa zozote kuhusu Rais. Kipi hasa tunachotaka kisijulikane? Na kwanini?

Sisi kama taifa tulitakiwa tuwe tumetoka huko kwenye hayo mazonge kutokana na tulipotoka.

Ni hayo tu!
 
Back
Top Bottom