Dr wa Manesi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 997
- 1,220
Napitia maoni ya haters wa mama Samia hapa, kiukweli Wana matatizo ya akili na kijinsia. Huo ndo ukweli.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nilisema tangu juzi hii safari imeratibiwa kipuuzi sana, wakati huu wa mvua za vuli maeneo ya caribean yanakuwa na vimbunga na mikondo ya bahari mikali, wakati huu wa uchaguzi marekani wako buzy na ushibdi wa trump wewe unaratibu safari ya rais kweli? hivi kweli kiswahili tu ndo kinatupeleka huko au na mambo ya tiba asili?Arudi tu home,asije tumbukia baharini bure!
laiti kingemkuta anatua huenda tungefurahi.TAARIFA KWA UMMA
KUAHIRISHWA KWA ZIARA YA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ILIYOKUWA IFANYIKE NCHINI CUBA
Havana, 07 Novemba, 2024
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuutaarifu umma kwamba ziara ya kitaifa ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyopangwa kufanyika tarehe 6 hadi 8 Novemba, 2024 nchini Cuba imeahirishwa.
Ziara hiyo imeahirishwa kufuatia taarifa rasmi iliyowasilishwa na Serikali ya Cuba ikitaarifu kuwa Cuba ingekumbwa na Kimbunga Rafael kuanzia tarehe 6 hadi 7 Novemba, 2024. Hali hiyo imepelekea Serikali ya Cuba kuchukua tahadhari ikiwemo kusitisha safari zote za ndege kuingia na kuondoka Cuba.
Pamoja na kuahirishwa kwa ziara hiyo, Mhe. Rais ameelekeza shughuli zote zilizopangwa kufanyika kipindi cha ziara yake ziendelee kuratibiwa chini ya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akishirikiana na Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Ziara nyingine ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Cuba itapangwa siku za usoni baada ya nchi hizo mbili kukubaliana wakati sahihi wa ziara hiyo
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
PIA SOMA
- Rais Samia kuisimamisha Dunia kutokea Cuba hapo Kesho
- Waziri Kombo aongoza kikao cha maandalizi ya ziara ya Rais Samia nchini Cuba
sio wote tusiokubaliana na hii safari tuko against mama, usitulishe maneno, hili eneo maarufu kama baracuda sio salama kukatiza kipindi hiki cha kuelekea masikaNapitia maoni ya haters wa mama Samia hapa, kiukweli Wana matatizo ya akili na kijinsia. Huo ndo ukweli.
Acha aende akatize huenda akakutana na Magu huko.sio wote tusiokubaliana na hii safari tuko against mama, usitulishe maneno, hili eneo maarufu kama baracuda sio salama kukatiza kipindi hiki cha kuelekea masika
"Force majeure"Si walisema atasimamisha dunia imekuaje tena [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.Acha aende akatize huenda akakutana na Magu huko.
😂😂 Dunia ndio imemsimamisha sasa.Si walisema atasimamisha dunia imekuaje tena [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Bado sijachelewa. Kwani Magu alikwenda Cuba au huko anakopaswa kwenda huyo mungu wenu?Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.
Saa hizi yupo Kizimkazi anashushia matofaha ya kiunguja kwa tende shake. Baada ya kupiga mishkaki ya chaza na mayai ya samaki iliyojaa filfil mdwawiya.
Dua ya kuku...Bado sijachelewa. Kwani Magu alikwenda Cuba au huko anakopaswa kwenda huyo mungu wenu?
Hii ni dua ya baba yako kuwa rahis wetu mungu mkuu aishi mileleDua ya kuku...
Imesimama. Huoni kuna mawingu nje na nyota hazionekani.😂😂 Dunia ndio imemsimamisha sasa.
Huyu anao uwezo wa kukiamrisha hicho kimbunga kusitisha shughuli zake hadi hapo mungu wake angemaliza ziara!
Kasimamisha Cuba. Anga la Cuba limefungwa.Si walisema atasimamisha dunia imekuaje tena [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
07 November 2024
Wakuu wa nchi za SADC kukutana kuhusu uchafuzi wa uchaguzi uliofanyika Msumbiji 9 Oktoba 2024
View: https://m.youtube.com/watch?v=NDREWSW3HKk
Wakuu wa Nchi kutoka kanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika watakutana kwa mkutano wa ajabu nchini Zimbabwe wiki ijayo kujadili uchaguzi wa hivi majuzi nchini Msumbiji.
Upinzani umekataa matokeo ya uchaguzi na kuitisha maandamano nchi nzima. Mitaa ya Msumbiji, hasa katika mji mkuu, Maputo, imeshuhudia kuzuka kwa ghasia. Viongozi hao pia watahutubia uchaguzi uliomalizika hivi punde nchini Botswana na uchaguzi ujao nchini Namibia
TOKA MAKTABA :
MIZENGO PINDA NA WAANGALIZI WA UCHAGUZI WAWASILISHA FAILI LA MAFANIKIO YA BOTSWANA
Chama dola kongwe cha Tanzania kijitayarishe, wanae Mizengo Peter Pinda
Botswana
MHESHIMIWA PINDA AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC JIJINI GABORONE
23 Oct 2024
Mkuu wa Missoni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Elias Magosi walipokutana jijini Gaborone, Botswana, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa.