Rais Samia aahirisha ziara yake ya Cuba

Rais Samia aahirisha ziara yake ya Cuba

Napitia maoni ya haters wa mama Samia hapa, kiukweli Wana matatizo ya akili na kijinsia. Huo ndo ukweli.
 
Arudi tu home,asije tumbukia baharini bure!
nilisema tangu juzi hii safari imeratibiwa kipuuzi sana, wakati huu wa mvua za vuli maeneo ya caribean yanakuwa na vimbunga na mikondo ya bahari mikali, wakati huu wa uchaguzi marekani wako buzy na ushibdi wa trump wewe unaratibu safari ya rais kweli? hivi kweli kiswahili tu ndo kinatupeleka huko au na mambo ya tiba asili?
 
TAARIFA KWA UMMA

KUAHIRISHWA KWA ZIARA YA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ILIYOKUWA IFANYIKE NCHINI CUBA

Havana, 07 Novemba, 2024

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuutaarifu umma kwamba ziara ya kitaifa ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyopangwa kufanyika tarehe 6 hadi 8 Novemba, 2024 nchini Cuba imeahirishwa.

Ziara hiyo imeahirishwa kufuatia taarifa rasmi iliyowasilishwa na Serikali ya Cuba ikitaarifu kuwa Cuba ingekumbwa na Kimbunga Rafael kuanzia tarehe 6 hadi 7 Novemba, 2024. Hali hiyo imepelekea Serikali ya Cuba kuchukua tahadhari ikiwemo kusitisha safari zote za ndege kuingia na kuondoka Cuba.

Pamoja na kuahirishwa kwa ziara hiyo, Mhe. Rais ameelekeza shughuli zote zilizopangwa kufanyika kipindi cha ziara yake ziendelee kuratibiwa chini ya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akishirikiana na Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Ziara nyingine ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Cuba itapangwa siku za usoni baada ya nchi hizo mbili kukubaliana wakati sahihi wa ziara hiyo



Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

PIA SOMA
- Rais Samia kuisimamisha Dunia kutokea Cuba hapo Kesho

- Waziri Kombo aongoza kikao cha maandalizi ya ziara ya Rais Samia nchini Cuba
laiti kingemkuta anatua huenda tungefurahi.
 
sio wote tusiokubaliana na hii safari tuko against mama, usitulishe maneno, hili eneo maarufu kama baracuda sio salama kukatiza kipindi hiki cha kuelekea masika
Acha aende akatize huenda akakutana na Magu huko.
 
07 November 2024

Wakuu wa nchi za SADC kukutana kuhusu uchafuzi wa uchaguzi uliofanyika Msumbiji 9 Oktoba 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=NDREWSW3HKk
Wakuu wa Nchi kutoka kanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika watakutana kwa mkutano wa ajabu nchini Zimbabwe wiki ijayo kujadili uchaguzi wa hivi majuzi nchini Msumbiji.

Upinzani umekataa matokeo ya uchaguzi na kuitisha maandamano nchi nzima. Mitaa ya Msumbiji, hasa katika mji mkuu, Maputo, imeshuhudia kuzuka kwa ghasia. Viongozi hao pia watahutubia uchaguzi uliomalizika hivi punde nchini Botswana na uchaguzi ujao nchini Namibia

TOKA MAKTABA :
MIZENGO PINDA NA WAANGALIZI WA UCHAGUZI WAWASILISHA FAILI LA MAFANIKIO YA BOTSWANA

Chama dola kongwe cha Tanzania kijitayarishe, wanae Mizengo Peter Pinda

Botswana


MHESHIMIWA PINDA AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC JIJINI GABORONE​

23 Oct 2024
Mkuu wa Missoni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Elias Magosi walipokutana jijini Gaborone, Botswana, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa.

Kila kiongozi wa SADC anayekuja Tanzania wakati nchi yake inakaribia kipindi cha uchaguzi, lazima akirudi huko kwao mambo yaharibike. Tumeshuhudia Zimbabwe, na sasa Msumbiji, inaonekana maccm huwa yanawapa hawa majamaa mbinu chafu za wizi wa kura wakidhani zinaweza ku function kwenye kila taifa.
 
Back
Top Bottom