Rais Samia aambiwe Makamu wa Rais ni Mkubwa kwa Rais wa Zanzibar, au anafanya makusudi!?


Umeniwahi mkuu. Nakumbuka sana hii kauli.
 
Wewe nawe ni zero brain. Mmoja anaitwa Rais na mwingine makamu wa rais bado huoni tofauti?
Makamu wa rais analinganishwa na makamu mwenzake.
Nahisi ulishawahi kufanyiwa surgery ya ubongo sio bure.
 
Kimuungano Mwinyi ni namba tatu.
Rais Jmhr no 1.
Makamu wa Rais no 2.
Rais Zanzibar no 3.
Spika no 4.
Jaji mkuu no 5.
Jaji mkuu Zanz no 6
Waziri mkuu no 7.
Makamu wa 1 zanzibar no 8
Makamu wa 2 zanzibar no 9
Naibu spika Tz no 10
Spika baraza la mapinduz no 11
Katibu mkuu kiongoz bara 12.
Katibu mkuu kiongoz zanz 13

Ila tukiwa huku Tz
Rais no 1
Makamu no 2
Spika no 3
Jaji mkuu no 4
Wazir mkuu no 5
Katibu mkuu kiongoz no 6

Marekebisho nipo tayari.
Kusema kweli mama anaona Mwinyi ni Rais ni kama hivo kuna kujisahau tu atajirekebisha.
 
Mkuu mwache Mama afanye yake kwa nafasi. Hivi tumeshasahau mara hii yaliyoji Chato kwa niaba ya Watanzania!
 
Nilihoji kwanini Samia amteue Mwinyi kuwakilisha mkutano wa SADC wakati mwinyi anaingia kwenye serikali ya muungano kama waziri, pia tuna makamu wa rais, waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje. Kwa kifupi asituletee uzanzibar wake atabaki one term president
 
Soma katiba ya muungano iliyofanyiwa marekebisho baada ya mfumo wa vyama vingi, rais wa Zanzibar ni mjumbe wa baraza la mawaziri, kwa muungano ni waziri sio zaidi ya hapo
 
Hayo ni mawazo yako au ni ibara gani ya Katiba?
 
Wakati wa kujadili umuhimumu wa muungano umefika. Hauna faida kwa Watanganyika
 
Angalia kiti chake huwa kinakaa wapi ?
Katiba bado inamtambua yeye ni no:3
Kasome katiba usiwe unasubiri kusimuliwa hata kiti kingekaa pembeni au chumbani kwa rais.
Hivi unafahamu ni kina nani wanateuliwa kukaimu nafasi ya rais endapo rai wa muungano ni mgonjwa au amepata matatizo, ukishajua utaelewa kwanini yule ni waziri kwa sababu hajatajwa kuna spika, jaji mkuu lakini yeye hayumo.
Mnataka katiba mpya wakati hii iliyopo hamuielewi.
 
Hapana, kiprotokali Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yuko juu ya Rais wa Zanzibar maana huyu ni mjumbe wa baraza la mawaziri wakati Makamu wa Rais anakuwa M/kiti endapo Rais hayupo.

Hata ukitazama mpangilio wa misafara ya viongozi utaona hilo maana iko hivi;
E1 (Escort number 1) msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
E2 (Escort number 2) msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
E3 (Escort number 3) msafara wa Rais wa Zanzibar.
E4 (Escort number 4) msafara wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
Watu wa Itifaki wamsaidie mh Rais asije akazua sintofahamu bila sababu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…