Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Kwanza, hapakuwepo utashi wa kisiasa kulifanya eneo lote la Ngorongoro kuwa Human Free.
Pili, wakazi wa maeneo hayo wapo, na sijui kama wameshirikishwa.
Tatu, Govt Decrees bila utashi wa kisiasa, unakuwa hugely unpopular.
Nne, watanzania kwa ujumla wamepigwa butwaa nauamuzi huo wa serikali ambao kimsingi unawapiga marufuku watu kuishi maeneo ya Ngorongoro bila kueleza sababu za kimsingi.
Tano, tunakumbuka Operation Vijiji vya Ujamaa mwanzoni mwa miaka ya 70. Rais Aboud Jumbe Mwinyi alifanyiwa fujo mbele ya uso wake kule Kyela, Mbeya, serikali ilipotaka kuwahamisha wananchi kwa lazima kwenda viijiji vya ujamaa na kwa kutumia nguvu.
Sita, tunaelekea mwaka wa uchaguzi. Serikali iliyopo madarakani inategemea nini katika hili, an unpopular move creates unnecessary resentment?
Saba, mama Samia lazima ujue ushauri unaopewa kuhamisha wamasai Ngorongoro utakuwa na matokeo ya kudhuru kisiasa. Wanaokushauri mwishowe hawataubeba msalaba wako.
Mimi ni kada wa CCM, na baada ya Magufuli nilimuunga mkono sana juhudi za mama Samia.
Lakini kwa hili la sasa, mama Samia lazima kula ile waingereza wanasema " a humble pie" au kukubali yaishe. Achana na mpango wa kuwahamisha wamasai Ngorongoro kwa nguvu.
Pia soma:Kuelekea 2025 - Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe
UPDATE
Rais wa JMT Mama Samia, ameagiza huduma za kijamii kurejeshwa huko Ngorongoro. Hii ni dalili njema kuwa Mama Samia kasikia kilio cha wananchi juu ya kuhamishwa kwa nguvu wananchi w jamii ya kimasai huko Ngorongoro.
Huu ni mwanzo mzuri nami kama Jidduzz nampongeza kwa dhati mama kwa kutoweka pamba masikioni.
View: https://x.com/MwananchiNews/status/1826969657221210495?t=EamN1_XX-Zk3EdiaHy7xAA&s=08