Suala la kuhamisha watu wote Ngorongoro halijapokewa vizuri na si tu jamii ya wamasai, bali watanzania kwa ujumla.
Kwanza, hapakuwepo utashi wa kisiasa kulifanya eneo lote la Ngorongoro kuwa Human Free.
Pili, wakazi wa maeneo hayo wapo, na sijui kuwa wameshirikishwa.
Tatu, Govt Decrees bila utashi wa kisiasa, unakuwa hugely unpopular.
Nne, watanzania kwa ujumla wamepigwa butwaa nauamuzi huo wa serikali ambao kimsingi unawapiga marufuku watu kuishi maeneo ya Ngorongoro.
Tano, tunakumbuka Operation Vijiji vya Ujamaa mwanzoni mwa miaka ya 70. Rais Aboud Jumbe Mwinyi alifanyiwa fujo mbele ya uso wake kule Kyela, serikali ilipotaka kuwahamisha wananchi kwa lazima kwenda viijiji vya ujamaa kwa nguvu.
Sita, tunaelekea mwaka wa uchaguzi. Serikali iliyopo madarakani inategemea nini katika hili, an unpopular move?
Saba, mama Samia lazima ujue ushauri unaopewa kuhamisha wamasai Ngorongoro ni lazima utakudhuru. Wanaokushauri mwishowe hawatabeba msalaba wako.
Mimi ni kada wa CCM, na baada ya Magufuli nilimuunga mkono sana mama Samia. Lakini mama Samia lazima kula ile waingereza wanasema " a humble pie" au kukubali yaishe. Achana na mpango wa kuwahamisha wamasai Ngorongoro kwa nguvu.
Pia soma:
Kuelekea 2025 - Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe