1. Ninaona pale
Kigoma Ujiji kamtoa
Mwantum Mgonja. Bibie alikuwa na ugomvi na madiwani wa Manispaa. Kumbuka Madiwani ndiyo mabosi wa Halmashauri kwa hiyo Wakurugenzi hawana budi kufuata maagizo yao.
2. Pale
Manispaa ya Ubungo kamtumbua
Elias Ntirihungwa ambaye alionekana kuelemewa na uzito wa Halmashauri ile yenye miradi mingi na kampeleka Mkurugenzi mpya anayetoka Jiji la Mwanza. Bwana
Elias aliingia Ubungo June 2023 lakini madudu ni mengi sana, na hata wakati anapewa kijiti ma Mtangulizi wake Beatrice, Bwana Elias alikiri viatu vya Bite ni vikbwa sana. Hatimaye Mapato ya Halmashauri yameshuka haswa pale
Magufuli Bus Terminal* na Mama kamuwasha kibao.
3. Lakini pia aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mr. Komba kahamishiwa Wilaya ya Geita. Za chini chini ni kwamba Bwana Komba alishindwa kabisa kufanya kazi na Mkurugenzi Elias, na kutamani Bi. Beatrice arudi, maana pigo la kwanza lilikuwa kushuka kwa mapato. Ikumbukwe Bi. Beatrice alikuwa Mkurugenzi Ubungo kwa miaka mitano na kufanya makubwa ikiwemo mapato kupanda kutoka Bi 5 mwaka 2018 hadi Bi 34 2023.
Sasa naona Mama hana nongwa na Bwana Komba na kaamua amsaidie Wilayani Geita ila akaachana na Bwana Elias Ntirihungwa aliuekuwa Mkurugenzi kishoia, na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ubungo ni kijana mdogo na Katibu wa zamani wa Chipukizi Taifa Bwana Hassan Bomboko.
4. Huko Mlimba naona mama kaachana na Rose Robert Manumba ambaye ni mtoto wa DCI wa zamani (RIP) Robert Manumba.
Lakini kule Tanga Jiji ninaona viatu vimekuwa vipana kwa Saidi Majaliwa na hatimaye kapewa Mji Mdogo wa Kondoa
View attachment 2929275View attachment 2929277
Mkurugenzi wa Kigoma Ujiji alidiriki hata kupost habari za kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani ila katoka yeye
View attachment 2929288