Rais Samia afanya Mabadiliko madogo ya uongozi Serikalini, amteua Daniel Chongolo kuwa Mkuu wa mkoa wa Songwe

Lucas Apelekwe Mbuga Ya Serengeti akalinde Simba wasile Swala.
 
Namie ngoja nimpelekee Samia cv yangu. Mtaani njaa kali.
 
Sijaona anayechukua nafasi ya Majaliwa Tanga, na pia alikopelekwa aliyekuwa DC wa Muheza.
Kutoka ukuu wa mkoa hadi ukurugenzi wa shirika.
Huyo alianza mbali au umemsahau alikuwa DG TTCL akahamishwa na mama akapelekwa somgwe kuwa Mkuu wa Mkoa akahamishwa Somgwe akapelekwa Tanga u-RC ndo leo unamuona kapelekwa UDART
 

Rose Manumba yupo Malinyi dc na sio Mlimba dc.
 
Uhamisho huo utaicost sirikali mabilioni ya fedha!
Uhamisho mmoja unajenga jumba kabisa dah... Kodizetu hizi.
Serikali ingekuwa inawabebea kilakitu Kwa gari zao kuhamisha hamisha watendaji wake tofautii na kulipana mabilioni kilamara!!
This country is very sick...
 
Huu ndio utaratibu tusioutaka..

Watu hawa i.e Ma RCs na DCs wanapaswa kuchaguliwa kwa kupigwa kura na wananchi..

Na wakishachaguliwa wanapaswa kukaa miaka mi5 ktk maeneo yao ya utawala ili wasimamie sera na mipango yao ya maendeleo waliyoinadi kwa wananchi ktk mikoa au wilaya zao..

Huu utaratibu kuteuana na kuhamishana hovyo hovyo haufai hata kidogo na unachelewesha maendeleo ya wananchi..

Kuna baadhi ktk orodha hiyo waliteuliwa na wengine kuhamishwa juzi tu hata hawajamaliza mwaka, mara tena wanahamishwa vituo vyao. Kwa utaratibu huu, huyu mtu hata kama alikuwa na mipango yake si ndio inakuwa imeishia hapo?

Hii ni kweli kabisa. Kwa sababu kwa utaratibu wa utawala wa kisheria na kikatiba tulionao, hawa viongozi wa kuteuliwa na wa kuchaguliwa, wakishaondoka ktk nafasi zao za uongozi ktk maeneo yao, kama Kuna jambo la kimaendeleo walilianzisha, nalo linakuwa limefia hapohapo..

Kwa utaratibu huu hatutafika popote au tutakuwa tunapiga hatua za taratibu sana za kimaendeleo...!
 
Kwanza ni gharama kubwa sn kwa wananchi, mwaka jana mwezi 6 kafanya uteuzi mkubwa baada ya miezi 8 watu wanabadilishwa tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…