Rais Samia Suluhu ameagiza Mawaziri kusimamia fedha za UVIKO-19 ili ziweze kutumika vizuri kwa kuwa mwisho wa matumizi yake ni Juni 2022, kama hazitatumika kwa 90% basi fedha zijazo kwa ajili ya miradi hiyo hazitapatikana au zitapungua
-
Amesema "Bado nasoma kuna tenda zinacheleweshwa TAMISEMI, vitu vya kuagizwa vya Wizara ya Afya na Wizara ya Maji ziagizwe. Kuna tenda zinazungushwa, watu wanasubiri rushwa na wengine wamegewe kidogo"
-
Rais amefafanua "Kuna fedha zinasubiri tumalize kuzitumia hizi za sasa ili hizo nyingine ziingie. Tusipovuka 90% hatutapata nyingine au tutapata kidogo kwani itamaanisha uwezo wetu ni mdogo. Simamieni ili zilizopo kwenye bomba ziweze kutema muda ukifika"
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣