Rais Samia afanya uteuzi, Kafulila awa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)

Rais Samia afanya uteuzi, Kafulila awa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)

[emoji38][emoji38] huyu kujifanya anajua kila kitu ndio kunamponza , nyuzi zake lazima achanganye kiswahili na lugha ya kigeni ili kuwachanganya wajinga wajue ni msomi sana , kumbe kwao ni Buzuruga bondeni kwenye mawe .
MKUU buzuruga ni ni city center Tena mjini kabisa sizani kama paschal mayalla alishawahi kufika maana yeye kwao vijijini kabisaa kwenye fisi wengi pamoja na ndugu Yake jiwe (WASHAMBA)
 
Inaonekana kazi ya uteuzi imeshafanyika mama anaachia tu " press release "
 
Humu jukwaani walikua wanamponda kua akalime pilipili na nyanya, bora aende huko akakusanye mtaji. Nna uhakika sasa hv hatafanya makosa tena maana fedheha ya kupigwa chini ilikua kubwa
Alifanya makosa gani Simiyu?
 
Chawa wa Mama hao
Kama ulivyo wewe chawa wa mbowe, siku si nyingi unaweza kula shavu la kuwa unamsindikiza mbowe ikulu ambako utakuwa na kazi ya kumuandikia minutes za vikao vyake na Mama Samia
 
Kuna shida kubwa sana serikalini kuliko tunavyodhani.
Acheni kukuza mambo yasiyo na msingi...a simple mistake ya kiuandishi kama hiyo ndio ireflect the " so called shida kubwa serikalini"...stop this nonsense.
 
Wadau,
Mkeka wa teuzi zingine huu hapa na Mstaafu Kafulila amekumbukwa!View attachment 2470231
View attachment 2470232

=====

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

Amemteua Dkt. Ellen Mkondya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa - Muhimbili. Dkt. Mkondya ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Amemteua Bw. Justine Peter Mwandu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC). Bw. Mwandu ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Reinsurance (TANRE).

Amemteua Prof. Verdiana Grace Masanja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI). Masanja ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.

Amemteua Bw. Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Bw. Mwakapeje alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria. Bw. Mwakapeje anachukua nafasi ya Bw. Casmir S. Kyuki ambaye atamaliza kipindi chake tarehe 07 Januari, 2023.

Amemteua Bi. Fatma Mohamed Abdallah kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Puma Energy Tanzania. Bi. Abdallah ni Meneja wa Kampuni ya Puma Energy nchini Geneva. Aidha, Bi. Abdallah anachukua nafasi ya Dominic Dhanah ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Bw. David Zacharia Kafulila kuwa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP). Bw. Kafulila ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mstaafu.

Teuzi hizi zinaanza mara moja.
Kumbe Samia na Magufuli hawana tofauti sana, uchawa wa Kafulila imemrudisha kazini. Njia pekee ya kupata uteuzi ni kusifia mamlaka ya uteuzi hata inapoboronga
 
Kujikomba katika sioasa za Bongo kunalipa
Uchawa utaharibu taifa hili kwa miaka mingi sana. Ni zimwi litakalotutafuna kwa karne nyingi sana. Sijawahi kushuhudia uchawa wa kiwango hiki kuanzia awamu ya mkapa hadi kikwete, huu ni uchawa wa hali ya juu sana na inaelekea raisi anapenda
 
Back
Top Bottom