Rais Samia afanya uteuzi. Katibu Mkuu Kiongozi ahamisha Vigogo 5 TANESCO

Rais Samia afanya uteuzi. Katibu Mkuu Kiongozi ahamisha Vigogo 5 TANESCO

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, alichukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka

Kabla ya uteuzi huo, Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Afrika Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi

Vilevile, Rais Samia amemteua Omari Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO

====

Rais Samia amemteua Hassan Seif Said kuwa Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kabla ya uteuzi, alikuwa Meneja wa Kanda Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TANESCO

Aidha, Michael Minja ameteuliwa kuwa Kamishna wa Petrol na Gesi, Wizara ya Nishati. Kabla ya kuteuliwa, Minja alikuwa Mkurugenzi Mkuu TIPPER

Vilevile, Rais amemteua Felschemi Mramba kuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu

=====

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amewahamisha Watumishi Waandamizi watano kutoka TANESCO kwenda Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo watapangiwa majukumu mengine

Waliohamishwa ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji, Khalid James; Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Masoko, Mhandisi Raymond Seya na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji, Mhandisi Isaac Chanje

Wengine ni Nyelu Mwamaja (Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi) na Amos Ndegi (Mwanasheria wa TANESCO)

View attachment 1952485

View attachment 1952487

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Mwenye CV ya Mr Maharage Chande Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO tafadhali.
 
Nani alikua less qualifued wakati Magu alikua anateua maprofesa tu, ama na hao ni less qualifued?

Hii ya kusema Magufuli aliteua wote kanda ya ziwa ni uongo pia. Magufuli anawwza kusemwa kwa mambo mengine mabaya ila sio ya ukabila. Hii ni kampeni ilianzishwa na watu wa kaskazini hasa wachaga kumchafua Magufuli ila haikua kweli.
Usisingizie ukaskazini magufuli alikuwa na favoratism sana na kubeba wakanda yake sasa wanawekwa wengine mnalia lia tu nakulalamika as usual, huyo Waziri alikuwa wa kanda gani, igp, mkuu wa majeshi, mkurugenzi wa TRC, wakurugenzi wa wilaya je?
 
Kuna ubaya gani Kama kazi wanafanya na hawatuteki?
Mbona Magu alijaza wasukuma wakawa wanatuteka na kutulazimisha tuwaabudu?

Mkristo akiwa na roho mbaya ana tofauti gani na Muslims mwenye roho mbaya?
Sukuma gang walikuwa hatari tulishuhudia viroba vya watu vikitupwa baharini hofu ilikuwa kila corner heri hata Hawa wavaa makobasi kama hawaonei watu
 
Mwenye CV ya Mr Maharage Chande Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO tafadhali.

Yaani nilikusahau hua anaanza wa kusifia ambae hata alieteuliwa hamjui utasikia jamaa ni kichwa sana, halafu wanafuata wanaoulizia dini ya alieteuliwa, halafu wanafuata wale wanaosema hapo hakuna kitu tumepigwa, halafu hua mnamalizia ninyi wa kuulizia CV huku ukiwa na degree ya ualimu unaulizia cv ya DG wa tanesco yaani wewe unaanza vetting baada ya uteuzi
 
Hawa watu Wengi Magufuli aliwapiga Haieleweki sababu ingawa pia wengine walionewa cha msingi tu wasituharibie Tukaanza Mgao.

Makamba ni balaa anakuchekea huku anakuuma.
 
Sukuma gang walikuwa hatari tulishuhudia viroba vya watu vikitupwa baharini hofu ilikuwa kila corner heri hata Hawa wavaa makobasi kama hawaonei watu
Samia ana mapungufu mengi ila ni bora kuliko yule aliyetaka tumwabudu
Yaan wengine walimwita yesu
Wengine wakamtaka Mungu amshukuru.
Hata kila idara akiwa Muslims ni sawa ili mradi wasituletee Mambo ya Magu.

Jirani msukuma anafanya kazi usalama basi na yeye mtaa ulilazimika kumuabudu
 
Si ni juzi tu January aliwapiga mkwara TANESCO, imekuwaje tena anaibadilisha timu ile ile kabla hawajavurunda? Alikuwa hajui kuwa anaenda kuibadilisha? Na ule mkwara unawahusu hii timu mpya pia au?
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, akichukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka

Kabla ya uteuzi huo, Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Afrika Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi

Vilevile, Rais Samia amemteua Omari Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO

====

Rais Samia amemteua Hassan Seif Said kuwa Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kabla ya uteuzi, alikuwa Meneja wa Kanda Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TANESCO

Aidha, Michael Minja ameteuliwa kuwa Kamishna wa Petrol na Gesi, Wizara ya Nishati. Kabla ya kuteuliwa, Minja alikuwa Mkurugenzi Mkuu TIPPER

Vilevile, Rais amemteua Felschemi Mramba kuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu

=====

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amewahamisha Watumishi Waandamizi watano kutoka TANESCO kwenda Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo watapangiwa majukumu mengine

Waliohamishwa ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji, Khalid James; Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Masoko, Mhandisi Raymond Seya na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji, Mhandisi Isaac Chanje

Wengine ni Nyelu Mwamaja (Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi) na Amos Ndegi (Mwanasheria wa TANESCO)

View attachment 1952485

View attachment 1952487

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Kweli kazi iendelee
 
Malizia na wale wnaouliza dini ya alieteuliwa hapa nikuangalia tu unakaa kimya kipindi cha magu usingewaona wanauliza dini dunia ina mambo hii acha kabisa
Hahaha bora mtu uwe neutral tu

Ova
 
Back
Top Bottom