Rais Samia afanya uteuzi. Katibu Mkuu Kiongozi ahamisha Vigogo 5 TANESCO

Rais Samia afanya uteuzi. Katibu Mkuu Kiongozi ahamisha Vigogo 5 TANESCO

Mkuu naomba nikumbushe huyu jamaa amewahi kuwa nani huko nyuma Hilo jina sio geni kwenye medani ya uongozi...
Ndio alikuwa MD wa TANESCO kabla ya Mwinuka huyu aliyeondolewa leo.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, akichukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka

Kabla ya uteuzi huo, Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Afrika Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi

Vilevile, Rais Samia amemteua Omari Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO

====

Rais Samia amemteua Hassan Seif Said kuwa Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kabla ya uteuzi, alikuwa Meneja wa Kanda Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TANESCO

Aidha, Michael Minja ameteuliwa kuwa Kamishna wa Petrol na Gesi, Wizara ya Nishati. Kabla ya kuteuliwa, Minja alikuwa Mkurugenzi Mkuu TIPPER

Vilevile, Rais amemteua Felschemi Mramba kuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu

=====

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amewahamisha Watumishi Waandamizi watano kutoka TANESCO kwenda Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo watapangiwa majukumu mengine

Waliohamishwa ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji, Khalid James; Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Masoko, Mhandisi Raymond Seya na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji, Mhandisi Isaac Chanje

Wengine ni Nyelu Mwamaja (Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi) na Amos Ndegi (Mwanasheria wa TANESCO)

View attachment 1952485

View attachment 1952487

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app

Hongera Mama Samia kwa kufuata ushauri muhimu
 
Hapo ndio watu wengi wanakosea. Level ya MD haihitaji elimu ile taaluma. Hapo ni suala la umahiri wa uongozi tu. Namna gani ataangalia v
CV za wale wasaidizi wake na kuwapangia majukumu.
Hapo ni leadership and management combined. Sio elimu ya electrical.
Tumewahi kuwa MD wa Muhimbili ambaye hakuwa Daktari.
Nikweli watu hawaelewi.
Mfano kipindi akiwa Dr Idrisa Rashid MD wa TANESCO alifanya vizuri sana wakati yeye sio mtaalam wa Umeme. Kumbuka huyu alikuwa Governor wa BOT.
 
Kweli kabisa wacha wajae tu at least huwezi kusikia kashfa na wizi ule wa escrow na EPA na wengine kugawana pesa mpaka kwa viongozi wakubwa wa dini yako hiyo

Umejaza server kwa mambo ya hovyo sana

Acha discrimination against Islam
Hautafaidi kitu
Ukweli unajulikana ni nani wamekula keki ya nchi kwa miaka tena bila aibu

Utakufa na roho mbaya
Sio roho mbaya mkuu Ila haya Mambo yanatakiwa yasijitokeze Sana yanaweza kutuletea shida baadae.
 
Waziri Makamba anahitaji TANESCO wajiendeshe kibiashara zaidi. Ngoja tuwape muda yawezekana wakafanya vizuri
IMG-20210925-WA0019.jpg
 
Nakubaliana na watu wanaosema January kaomba team yake ili abadilishe mambo.

People are gonna get hurt na TANESCO inaenda haribika like never before, this was always the danger with him ataleta ubunifu ambao hana.

The nonsense tu ya kusema wauze 20% ya hisa ili kulipa madeni. Wakati TANESCO inadaiwa sh/trillioni 5 na wanahisa ambazo wametenga for whatever nonsense reasons ambazo roughly ni million moja.

Sasa kuuza 20% ya hizo hisa ili upate sh trillioni 5 ata hisa moja ukiuza kwa million 1 upati hiyo income (jiulize watanzania wangapi kununua hisa laki mbili kwa millioni bei ya 1m kwa hisa). Besides ata ukilipa madeni yote kwa miujiza TANESCO CoS bado kubwa upati ata gross profit hasara ipo pale pale.

So hata ukinunua hisa usitegemee gawio mpaka management ijifunze kubalance operation cost maana hilo ndio tatizo la msingi.

Sasa jiulize boss wa mass media na energy ‘management ‘wapi na wapi’ safari hii hakuna copy and paste.

I am telling you hali inaenda kuwa mbaya zaidi TANESCO.

Binafsi nilitaka kuona January anapewa wizara ngumu tupime uwezo wake; ni wajinga wajinga tu wanaosifiana ujinga kule twitter.
 
Sidhani km ni afy kuwa na jicho la udini kiasi hicho unless unafanya harakati za kupigania dini yako itawale

Chamsingi tujaji kwa ueledi na uchapakazi wa muhusika regardless ni wa dini yako Au mwemzako

Udini ni dhana mbaya sana na itatutafuna mpaka tunaingia kaburini

Mimi ni Muslim lakini sikubaliani na huyu maza kwa sababu TU utendaji wake unalega lega but dini hainihusu HAPA

Tuwe na jicho la utendaji si udini mkuu
Udini Ni kitu mbaya Sana mkuu ndo maana inabidi itumike busara kubwa Sana hata kwenye promotion ya nafasi mbalimbali watu wasinuse hata harufu ya Jambo ilo watanzania tumejengwa kwa misingi ya umoja na mshikamo bila kujali itikadi zetu.
 
Samia ana mapungufu mengi ila ni bora kuliko yule aliyetaka tumwabudu
Yaan wengine walimwita yesu
Wengine wakamtaka Mungu amshukuru.
Hata kila idara akiwa Muslims ni sawa ili mradi wasituletee Mambo ya Magu.

Jirani msukuma anafanya kazi usalama basi na yeye mtaa ulilazimika kumuabudu
Mimi heri Samia mara elfu kuliko magufuli bana tulikuwa tunaishi kwa hofu mda wote full mauonevu aaargh, Bora maustaadhi huwa hawaonei mtu vibaya atleast huwa wako fair, hawapendi kusifiwa wala kuabudiwa aisee
 
Wakifanya hivyo bei zitakuwa hazishikiki. Waache tu kufanya siasa zao ndani ya shirika hilo na wawaachie management wafanye maamuzi bila kuingiliwa na maccm na watendaji wa Serikali pale madini na Ikulu.
That's practically impossible. Wateuzi na wanasiasa, CCM hao hao particularly kwa maana ndio wana dola. Watake wasitake lazima waangaliwe. Shirika haliwezi kiwa na ufanisi kwani hata akiingia mkurugenzi mpya na bodi mpya hawana time frame ya maono na utekelezaji, na hata akija raisi na waziri mwingine kesho na yeye anafumua tu kutokana na utashi wake.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Sio roho mbaya mkuu Ila haya Mambo yanatakiwa yasijitokeze Sana yanaweza kutuletea shida baadae.

Hakuna la kulaumu hapo
Kuna wakati wanachaguliwa Watu 10 kwa mfano na wanne wakawa na majina ya kiislam utaona comment zingine zinaanza kusema ooh waislamu wamekuwa wengi wakati ratio inaonekana kabisa wapi wengi

Hakuna udini bali utendaji wa kazi na hao pia walioteuliwa wameteuliwa na elimu zao na fani zao

Hebu nikuulize kwa matamko ya huyo ni ya uungwana au ni kutafuta maneno?

Anyway tuyaache maana huwa hatulalamiki hata wateuliwe nani
Mbona walipangwa safu nzima ya wasukuma na mkakaa kimya na kufungwa midomo na matusi juu

Tena wengine walitukanwa wakiwa mawaziri na kudhalilishwa na kuambiwa eti wakubwa kwangu ila nawaambia ni wapumbavu

Au umesahau
 
Back
Top Bottom