Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Popote alipo Ndugu ALBERT CHALAMILA naomba tafadhali aje hapa. Nimeandaa tafrija fupi ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa RC wa Mwanza.
Walimponda sana huyu Ndugu. Ukiwauliza, kosa lake ni nini? hawana majibu. Hongera sana Ndugu ALBERT CHALAMILA.
I feel sorry for you nadhan kabla ujafanya judgement na kuwatuhumu waliokuwa wanakosoa utendaji wa chalamila ungepaswa kujua watu wa mahali alipokuwa i mean mkoa wa Mbeya wanasemaje. Nipo mbeya kaka and mambo yanayoendelea Mbeya ni aibu mpaka kufika leo ni siku ya tano tukielekea wiki kuna mgomo wa daladala mkoani mbeya na sio mara ya kwanza kwasababu kuna madai ya msingi ambayo wanayadai lakin hayatimizwi and imagine RC yupo kimya kabisa as if hajui yeye ni RC na inasemekana anawaruhusu bajaj even kuvunja sheria coz nasikia anamiliki bajaj nying mjini aibu ilioje nadhan ifike muda watu wanaokuwa kwenye hizi nafasi wawe wanaajiriwa kama watumishi wengine wa serikali na sio uteuzi coz wanabweteka na kusahau majukumu yao kwasababu mwenyekiti wa chama yupo nyuma yao!!!!
 
Hi huyu Maneno Mbegu mme wa Queen Sendiga ana Uhusiano gani na Sudani Kusini? Kwenye picha ya harusi yao alikuwa amevaa tai yenye bendera ya Sudan Kusini!
1621096500981.png
 
Salaam Wakuu, Huu ndo uteuzi rais kafanya.

Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Bw. Mwakitalu kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Hamduni Mkuu wa TAKUKURU, Amos Makala kawa mkuu wa Mkoa wa Dar, Kafulila kawa mkuu wa Mkoa Arusha, Chalamila kawa mkuu wa Mkoa Mwanza, Queen Sendiga kawa mkuu wa Mkoa Iringa(Queen alikuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Uchaguzi wa Oktoba 2020), Makongoro Nyerere kawa mkuu wa Mkoa Manyara.

Chalamila kawa mkuu wa Mkoa Mwanza(Albert Chalamila alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya), Kunenge kawa mkuu wa Mkoa wa Pwani( Aboubakar Kunenge alikuwa Mmkuu wa Mkoa wa Dar), Kagaigai kawa mkuu wa Mkoa KIlimanjaro(Stephen Kagaigai alikuwa Katibu wa Bunge), Ali Hapi kawa mkuu wa Mkoa Tabora(Hapi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa). Anna Mngwira amesitaafu alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo atapangiwa kazi nyingine.

View attachment 1785850
View attachment 1785846
View attachment 1785849
Makala karibu DSM.
Makongoro nae amekumbukwa
 
Pale ulipomla kichwa mtu afu leo anashikilia kesi yako.....kweli Dunia duara.
 
Naona Mkuu wa JKT wa zamani Maj. General Charles Mbuge katolewa na kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera.

Maj. General Charles Mbuge anatakiwa ajitathmini sana utendaji wake na tabia zake za hovyo alizokuwa nazo akiwa JKT maana hiyo imekuwa ni demotion kwako.

Wakati wa utendaji wake akiwa Mkuu wa JKT Maj. Charles Mbuge alikuwa na mapungufu na natatuzo yafuatayo;

1. Kujipendekeza sana kwa mwendazake mpaka alifikia kuwadharau mabosi wake

2. Hata kupandishwa cheo kuwa Maj. General kulikuwa na walakini

3. Empties😆😆😆 za vijana waliokuwa wanakwenda JKT na hivyo kupelekea kuwa na malipo yaliyokuwa na walakini sana. Mh. Rais apeleke team ya wakaguzi kwenye makambi yote ili kukinganisha idadi halisi ya vijana waliokuwa wanapelekwa JKT na idadi ya pesa iliyokuwa inaombwa hazina
4. Alikuwa anaoenda kuwanyanyasa wale wote waliokuwa na mawazo tofauti kuhusu kumanage rasilimali fedha na hivyo kupelekea kuwahamisha vituo kama ishara ya kuwakomoa
6. Kuna badhi ya askari alikataa kuwapanxisha vyeo mwezi wa 2 wakati walikuwa wanastahili kutokana na chuki binafsi tu.

7. Kuna askari mmoja yuko Kigoma alitakiwa apandishwe cheo mwezi wa 2 kuwa Major lakini Maj. General Mbuge alilinyofoa jina lake wakati wa kuyapeleka majina Ngome ili kumkomoa askari husika kwa chuki binafsi tu

8. Maj. General Charles Mbuge kutokana na kutojiamini na ukizingatia kuwa na shule ndogo aliwagawa wafanyakazi wa JKT

Mwisho, atakaekuja kuchukua nafasi ya Maj. General Mbuge ajaribu kuangalia weakness alizokuwa nazo Mbuge ili kujenga team work na nidhamu kwenye jeshi letu, acha mambo ya kuonea watu.

Asante!!
Umeandika kama mtu chuki kwa maslahi binafsi au kikundi ! 😆
 
Wachagga wana nguvu kubwa ya kiuchumi nchi hii. Wanachotafuta ni nguvu ya kisiasa(mamlaka). Wakipata na jinsi wanavyopendana sana wao kwa wao, kuna athari itatokea kwa jamii zingine kubeba chuki dhidi yao ambayo yaweza kumature na kuwa tishio. Wachagga waachwe kwenye biashara kama wahindi na waarabu. Wapate nafasi ndogo ndogo tu.
Tushawajua toka mrema alipogombea mwaka 1995, yaani wale wabaguzi sana, walimharibia hata mrema, hawatapa uongozi wa nchi .Sasa waliyemfukuza chadema kaja kama mkuu wa mkoa kwenye ngome yao.Hongera Kafulila piga kazi
 
Salaam Wakuu, Huu ndo uteuzi rais kafanya.

Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Bw. Mwakitalu kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Hamduni Mkuu wa TAKUKURU, Amos Makala kawa mkuu wa Mkoa wa Dar, Kafulila kawa mkuu wa Mkoa Arusha, Chalamila kawa mkuu wa Mkoa Mwanza, Queen Sendiga kawa mkuu wa Mkoa Iringa(Queen alikuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Uchaguzi wa Oktoba 2020), Makongoro Nyerere kawa mkuu wa Mkoa Manyara.

Chalamila kawa mkuu wa Mkoa Mwanza(Albert Chalamila alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya), Kunenge kawa mkuu wa Mkoa wa Pwani( Aboubakar Kunenge alikuwa Mmkuu wa Mkoa wa Dar), Kagaigai kawa mkuu wa Mkoa KIlimanjaro(Stephen Kagaigai alikuwa Katibu wa Bunge), Ali Hapi kawa mkuu wa Mkoa Tabora(Hapi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa). Anna Mngwira amesitaafu alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo atapangiwa kazi nyingine.

View attachment 1785850
View attachment 1785846
View attachment 1785849
Hicho chama cha queen sendiga ADC ni chama kidogo cha chama tawala,nakumbuka uchaguzi uliopita kampeni meneja wa ugombea udiwani kwa tiketi ya ccm naye pia aligombea udiwani ADC,yaani huku ni kampeni meneja na huku anagombea ADC
 
Paul Makonda naye anaweza kukumbukwa kwenye awamu ya saba au ya nane. Aendelee tu kuwa mwadilifu na mvumilivu kwenye chama chake cha ccm kama hao wenzake walivyofanya.
Paul Makonda angeteuliws Mwanzs ingekuwa poa sana
 
Mama ilimradi tu afanye lolote aongolewe kwa miaka watu walikuwa wanalalama kubadilisha badilisha wakuu wa mikoa na wilaya kunaondoa consistencies ndio maana Magufuli aliwaacha.

Hao watu kwa muda waliokaa wanafahamu changamoto za maeneo yao, plan zilizokuwepo na changamoto za watendaji wao.

Kingine Magufuli for once alijitahidi kuweka wakuu wa mikoa kutokana na maeneo wanayoyafahamu au skills zao ili watatue changamoto kutokana priority wanazozifahamu wao.
Kama Mh. Mtaka kumuondoa Simiyu haijakaa sawa kabisa. Najua amepewa Dodoma kwa sababu ya uchapakazi wake ila Simiyu alikuwa na mambo mazuri ya kujenga mkoa mpya
 
Back
Top Bottom