Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya kustukiza katika soko la Kariakoo Dar es Salaam na kuongea na wafanyabisahara wa maeneo hayo
KARIAKOO
Rais Samia Suluhu amewatembelea na kuwasikiliza wanyabiashara wanaofanya biashara ndani ya soko la Kariakoo, baada ya matembezi Rais Samia alizungumza nao wote kwa pamoja.
Rais Samia: Nimeona nije nione mahali ambapo watanzania wengi wanafanya biashara, nimesikia baadhi ya malalamiko kwahiyo nikaona nije nione mlipo na mnavyofanya biashara zenu.
Nimefanya mahojiano na wachache ndani kati yenu lakini yamenipa sura ya soko linavyoendeshwa na sijui kama viongozi wa soko wako hapa.
Katika ziara yangu nimeona Serikali tusaidia kusimamia kufanya tathmini ya uendeshaji wa soko lote kwasababu hali niliyoiona ndani na hata nje kwenye vibanda hairidhishi.
Serikali pia kuanzia wakati mpendwa wetu Magufuli yupo hadi leo, nia yetu ni kusaidia wafanyabiashara wadogo wadogo. Naona usadizi kwa wafanyabiashara wadogo wadogo haupo ila kuna kutengeneza faida kwa uongozi wa soko au kwa shirika labda.
Jingine, nimeangalia bidhaa zilizomo ndani ni vurugu mechi, huoni bidhaa gani iko wapi, unakuta muuza vyerehani yupo katikati ya muuza madawa ya kilimo na dawa za panya na mambo mengine.
Wakati tunafanya tathmini ya soko, nimuagize na naambiwa waziri wa Tamisemi alitoa hayo maagizo, kusimamisha uongozi uliopo na tuwatake vyombo vya serikali vifanye uchunguzi kwanza halafu tutakuja kutoa maamuzi.
Kwa wakati huu naomba muendelee na biashara zenu kwa salama bila vurugu, serikali iko pamoja nanyi lakini na nyie ndugu zangu, wakati serikali inawabeba, wanasema bebweo hujikaza.
Wakati Serikali inawabeba nanyi jitahidini kufuata sheria zinazowekwa katika maeneo mlipo kwasababu nimeona njia zote zimezingirwa, vibanda kila pahali.
Kwahiyo nitakaa na uongozi wa Jiji nione njia nzuri ya kuwapanga na njia nzuri ya kugawa maeneo ya kufanyia kazi.
CCM hawajawahi kuacha Drama.
JIWE kaharibu hii nchi na yeyote atakaye jaribu kurudisha misingi ya awali atalaumiwa na kutukanwa.
NCHI IMEKUWA CHAFU sawa na choo cha stendi: Machinga wamepanga biashara barabarani, kila kona, service road, wameacha masoko tupu, watanzania tumekuwa kama ngombe, mtu anakula ugali barabarani hata kuku hawezi fanya hivyo, uchafu uchafu.
KIKWETE mzee wa msoga was very smart, unaweza fikiri mzungu, Mungu ampe miaka tujifunze kwake.
Nchi ilikabidhiwa kwa mshamba imekuwa hovyo kabisa.