Rais samia: Afrika imejaa fursa tele

Rais samia: Afrika imejaa fursa tele

Makonde plateu

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,443
Reaction score
3,480
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema ni lazima vijana wabadilishwe mitizamo yao juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana Afrika na kuondoa ile mitizamo ya kwenda nje ya bara hilo kutafuta maisha.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 26, 2023 katika mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika kuhusu rasilimali watu unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere Dar es Salaam.

Idadi kubwa ya vijana tulio nao Afrikia ni fursa ya pekee kwa mageuzi ya uchumi wetu, kuliko kuwaacha wavuke bahari wapigwe njiani wazamishwe, kwa ajili ya kusema kwamba wanakwenda Ulaya kutafuta maisha bora, maisha bora watayapata Afrika tukiwaendeleza,"amesema Samia

Aidha Rais Samia amesema ni lazima elimu ya uzazi itolewe kwa vijana ili kuendana na hali ya idadi ya watu ilivyo kwa sasa katika bara la Afrika.

Ni lazima tuwafundishe watoto wetu kuhusu uzazi wa mpangilio, Afrika tuna idadi kubwa sana ya watu na hii inaweza kutuletea tija au kutuletea mambo yasiyofaa kama hatutoitumia vizuri" amesema Samia.
 
Ni Kweli Lakini tunashindwa kujisimamia, Kwa mfano issues za bandari,,je Kuna haja ya kubinafsisha ????
 
Ni kweli ina fursa nyingi sema ufanisi ndio hakuna na ndio maana anaamka kiongozi asubuhi anaita wawekezaji wawekeze kwenye bandari zake zote milele
 
Afrika kumejaa ufala tu hakuna mwanga huku zaidi ya giza kama zilivyo ngozi zetu.

Hili lijinga sijui lina ongea nini ?
CUoqLDHWwAE8VgJ.jpg
 
Back
Top Bottom