Rais Samia: Afrika lazima inufaike na thamani ya Kahawa yake – Tunapata 0.5% tu ya Dola Bilioni 500!

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais Samia akifungua Mkutano wa 3 wa Nchi Zinazozalisha Kahawa Afrika Februari 22, 2025 Ukumbi wa JNICC Dar es Salaam


Wageni kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wakishiriki Mkutano wa Tatu wa Nchi Zinazozalisha Kahawa Barani Afrika, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Tanzania imepata nafasi ya kuwa mwenyeji wa mkutano huu kutokana na maboresho makubwa yaliyofanyika katika sekta ya kahawa nchini, ambapo sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza katika uzalishaji wa zao hilo barani Afrika. Uzalishaji umeongezeka kutoka wastani wa tani 50,000 hadi 85,000, sawa na ongezeko la asilimia 67 katika Awamu hii ya Sita.

Miongoni mwa maboresho yaliyopelekea ongezeko hilo ni pamoja na ugawaji wa miche zaidi ya milioni 20 kila mwaka kwa wakulima wa kahawa nchini, uchimbaji wa visima vya kumwagilia zao hilo mkoani Songwe, ununuzi wa mitambo mipya ya kuchakata kahawa mkoani Kigoma, pamoja na utoaji wa ruzuku za mbolea kwa wakulima katika maeneo yote yanayozalisha kahawa.

Hotuba ya Rais Samia

"Kahawa ni tamu sana na kinywaji kinachotuliza akili. Takwimu zote zinaonyesha kwamba kila siku watu wanakunywa vikombe vya Kahawa takribani bilioni 3 dunia nzima. Kati ya vikombe hivyo vipo vyenye Kahawa nzuri inayozalishwa na Wakulima wa Afrika wengi wao wakiwa ni wakulima wadogo."

"Jasho lao (Wakulima) limeleta tabasam kote duniani kupitia kinywaji hiki kizuri cha Kahawa, licha ya changamoto mbalimbali zinazokabili zao hili la Kahawa lakini uhitaji wake mkubwa duniani ni fursa kubwa sana kwa bara hili ambako zao hili limegunduliwa"

"Kabla sijaingia hapa niliingia kwenye Maonyesho na nikaona Kahawa inavyozalishwa, inavyongezwa thamani na nahadhi ya Kahawa yetu barani Afrika sasa hivi Ulimwenguni"

"Huko nyuma Kahawa yetu ilikuwa inaenda Ulimwenguni inaongezwa thamani inarudishwa kwetu tunanunua ghali, mpaka sasa hivi hali iko hivyo lakini nilichokiona kwenye maonyesho sasa tunakwenda kushindana kwenye uzalishaji, uwekezaji, uongezaji wa thamani ya Kahawa ndani ya bara la Afrika. Nimekuta vijana wametengeneza Kahawa kama tunayokunywa Ujerumani, Uingereza pamoja na naksh zile juu ya Kikombe. Vijana wetu sasa wanatuonyesha njia na sisi hatuna budi ya kuwapa nguvu na ushirikiano ili waweze kuendeleza Kahawa"

"Malengo yetu kama Tanzania tumesema ifikapo mwaka 2030 angalau "asilimia 20-25 ya Kahawa tunayozalisha tutakuwa tunaifanyia usindikaji hapa ndani"

"Kwenye mkutano uliopita wa jukwaa hili uliofanyika Kampala, kwenye mnyororo wa thamani wa Kahawa duniani unaokadriwa kufikia dola za Marekani bilioni 500, Afrika inaambulia asilimia 0.5 ya bilioni $500 ya biashara ya Kahawa duniani, yaani takribani dola bilioni 2.5. Zaidi ya asilimia 90 ya mapato yanayotokana na Kahawa inayozalishwa katika bara la Afrika inakwenda nje ya bara letu."

"Wazalishani ni sisi lakini faida inakwenda kwengine na sisi tunabakia Afrika kama shamba tu, kwamba kuna watu kule wana Shamba lao Afrika kazi yetu ni kuwalima, kuwavunia, tuwapelekee wafanye usindikaji alafu waturudishie kama tunavyofanya kwenye Pamba na mazo mengine"

"Changamoto ya tatu ni kiwango kidogo cha biashara baina ya nchi za Afrika zenyewe, licha ya kundi letu hili kuwa wazalishaji wa Kahawa na zaidi ya Asilimia 90 ya Kahawa hiyo kusafirishwa nje ya Afrika ukweli pia ni kuwa zipo nchi kadhaa barani Afrika ambazo ni waagizaji wakubwa wa Kahawa ndani ya Afrika yetu lakini biashara haifanyiki kati ya nchi zetu za Kiafrika, hapo tumepoteza fursa ya Kibiashara"
 
Tanesco wanamhujumu mama maana wamekata umeme tusijue raisi wetu anaongea nini.

Hivi umeme unakatwaje siku ya.mikutano muhimu
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi pamoja na wageni mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika (The 3rdG25 Africa Coffee Summit) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaamtarehe 22 Februari, 2025.
 

Attachments

  • VID-20250222-WA0189.mp4
    6.1 MB
  • VID-20250222-WA0188.mp4
    2.8 MB
  • VID-20250222-WA0187.mp4
    7.1 MB
  • VID-20250222-WA0186.mp4
    8.7 MB
  • VID-20250222-WA0185.mp4
    9.1 MB
  • VID-20250222-WA0184.mp4
    7.3 MB
  • VID-20250222-WA0183.mp4
    7.1 MB
  • VID-20250222-WA0182.mp4
    8.1 MB
  • VID-20250222-WA0181.mp4
    8 MB
  • VID-20250222-WA0180.mp4
    5.9 MB
  • VID-20250222-WA0179.mp4
    7.5 MB
  • VID-20250222-WA0168.mp4
    8.6 MB
Kichwa Cha habari kinatakiwa kisomeke rais mrithi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.maana hakuchaguliwa ispokuwa tu aliupata pasipo matarajio yake
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi pamoja na wageni mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika (The 3rdG25 Africa Coffee Summit) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaamtarehe 22 Februari, 2025.
Utatusimulia alichosema
 
Hivi kama taifa hatuwezi kumtoa huyu rais kwa mkopo?
 
Back
Top Bottom