Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifungua Kikao Kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa / Vikosi katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi, leo tarehe 30 Agosti, 2022.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania - IGP Camillus Wambura
Takwimu zinaonyesha kuongezeka kwa makosa makubwa ya jinai kutoka makosa 24848 katika kipindi cha Jan - Jun, 2021 hadi makosa 27623 katika kipindi cha Jan - Jun, 2022.
Takwimu zinaonyesha kuongezeka kwa ajali 97 kutoka ajali 858 katika kipindi Jan - Jun, 2021 na kufikia ajali 955 katika kipindi cha Jan - Jun, 2022 sawa na 11.3%. Ajali zilizosababisha vifo zimeongezeka kufikia 58 kutoka ajali 469 Jan - Jun, 2021 na kufikia ajali 527 Jan - Jun, 2022 Sawa na 12.4%, wingi wa ajali hizi chanzo kikitajwa kuwa mwendo kasi na uzembe wa madereva.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi - Hamad Masauni
Maboresho katika sehemu mbalimbali ikiwemo kwa jeshi la polisi ni muhimu sana katika kupunguza uhalifu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Samia Suluhu Hassan
Dunia inaendelea kubadilika kwa kasi kubwa katika matumizi ya teknolojia na sisi kama sehemu ya dunia hatuwezi kupitwa na mabadiliko hayo hasa ukizingatia wahalifu wanabadilisha mbinu zao kadri teknolojia inavyokuwa.
Jeshi la polisi lijirekebishe kwenye mambo mbalimbali ikiwemo;
- Uongozaji na uendeshaji wa jeshi la polisi: Kujirekebisha kwenye matumizi mabaya ya fedha za bajeti na mahusiano ya jeshi na wizara.
- TEHAMA: Kuhakikisha jeshi la polisi linaingia kwenye mfumo wa tehama haraka na kupewa mafunzo stahiki.
- Mafuta ngazi za mkoa na wilaya: Mafuta yanayolengwa kutumika na askari yatumike kwa lengo kusudiwa.
- Sare: Ieleweke jeshi la polisi linafanya kazi gani kwenye kuagiza na kusambaza sare, isiwe inafanywa kwa kificho.
- Mafunzo: Mafunzo yanayotilia mkazo kwenye uadilifu, maadili yatolewe kwa askari kuhakikisha wapatikana askari bora wenye weledi.
- Ubunifu: Mambo ya ubunifu yaende sambamba na jeshi la polisi, isiwe wanafanya kazi nje na kuwatoa kwenye lengo na kazi zao za kipolisi.
- Rushwa, uzembe: Jeshi la polisi lisimame imara na kushika nafasi yake kama jeshi.
- Maslahi ya askari: Manung'uniko ya askari yafanyiwe kazi ili askari wafanye kazi kwa weledi.
Ubambikaji wa kesi unaofanywa na jeshi la polisi kwa kutumia nafasi zao lishughulikiwe, kabla ya mtu kupelekwa ndani basi ihakikishwe kuna ushahidi wa kutosha.
Zanzibar kwa uhalisia wake ni eneo dogo, lipo wazi na hatarishi lenye jeshi la polisi dhaifu, hivyo linahitaji umakini wa kipekee kukabiliana na wahalifu wanaokimbilia huko kujificha, kuficha magendo na kufanya uhalifu kama kuficha madawa ya kulevya na biashara haramu ya kuuza binadamu(human trafficking). Lakini pia askari wapewe mafunzo wa kufanya kazi zao kwa kufuata maadili yao ya kazi.