technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 12,706
- 52,355
Wanamdanganya au anajidanganya mwenyewe ??Anaona kila kitu kipo sawa wanamdangana sana wasaidizi Wake
Hii haikubaliki kabisaa.Rais Samia afunguka ya Moyoni kuhusu kauli za Wahafidhina wa mfumo dume ambao hawakuwa na imani naye wakati anachukua nafasi ya Urais na waliothubutu kusema "Tuna Rais wakuambiwa afanye na mwenye maamuzi ya Kitchen Party" wakati akizungumzia nafasi ya Mwanamke katika Uongozi katika Siasa.
Akishiriki Madhimisho ya Miaka 10 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi katika Ukumbi wa The Super Dome Masaki Dar es Salaam, leo tarehe 21 Februari,2025, Samia amesema;
"Hapa nataka kusema ya Moyoni, kwenye wahafidhina wa mfumo dume kwamba wakati ule hakukua na imani kabisa, hakukua na imani au kuamini kwamba yule mwanamke anaweza kufika hapa [hakukua..]"
"Kuna waliothubutu kusema tuna Rais wakuambiwa fanya tu na atafanya. Kuna waliothubutu kusema hatuna Rais tuna House girl. Kuna waliothubutu kusema maamuzi ya Kitchen Party, yale ambayo nilikuwa nafanya"
Soma, Pia: Rais Samia: Nafasi ya Uongozi unayoipata Mwanamke isiwe sababu ya kuharibu familia
Rais Samia afunguka ya Moyoni kuhusu kauli za Wahafidhina wa mfumo dume ambao hawakuwa na imani naye wakati anachukua nafasi ya Urais na waliothubutu kusema "Tuna Rais wakuambiwa afanye na mwenye maamuzi ya Kitchen Party" wakati akizungumzia nafasi ya Mwanamke katika Uongozi katika Siasa.
Akishiriki Madhimisho ya Miaka 10 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi katika Ukumbi wa The Super Dome Masaki Dar es Salaam, leo tarehe 21 Februari,2025, Samia amesema;
"Hapa nataka kusema ya Moyoni, kwenye wahafidhina wa mfumo dume kwamba wakati ule hakukua na imani kabisa, hakukua na imani au kuamini kwamba yule mwanamke anaweza kufika hapa [hakukua..]"
"Kuna waliothubutu kusema tuna Rais wakuambiwa fanya tu na atafanya. Kuna waliothubutu kusema hatuna Rais tuna House girl. Kuna waliothubutu kusema maamuzi ya Kitchen Party, yale ambayo nilikuwa nafanya"
Soma, Pia: Rais Samia: Nafasi ya Uongozi unayoipata Mwanamke isiwe sababu ya kuharibu familia
Samia anafaa kuwa Rais hadi 2040,akitoka tumpe Abdul, watatuvusha mbali sana sana.Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu amesema wakati anachukua kijiti cha Urais kuna baadhi ya Watu (Wahafidhina wa Mfumo Dume) hawakuamini kwamba Mwanamke anaweza kuwa Rais na akaongoza vizuri na kwamba wapo walioenda mbali na kusema hatuna Rais tuna House Girl na maamuzi yake ni ya kitchen party lakini kwa sasa kwa kazi nzuri aliyofanya, Watu hao wote wamebadili mitazamo yao na wamekubali kuwa inawezekana Mwanamke akaongoza kiti cha Urais vizuri.
Rais Samia amesema hayo leo February 21,2025 wakati akiongea kwenye Maadhimisho ya Miaka 10 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Rais Samia amesema
“Bakari amesema kuna wakati kunja speech yako tuambie ya moyoni, hapa nataka kusema ya moyoni, kwenye Wahafidhina wa Mfumo Dume, wakati ule hakukuwa na imani kabisa, hakukuwa na imani au kuamini kwamba yule Mwanamke anaweza kufika hapa, kuna waliothubutu kusema tuna Rais wa kuambiwa fanya tu na atafanya, kuna waliothubutu kusema hatuna Rais tuna House Girl, kuna waliothubutu kusema maamuzi ya kitchen party yake ambayo nilikuwa nafanya, kwahiyo unaweza kuona imani ya wenzetu anaposimama Mwanamke”
“Lakini leo nadhani wote wamebadilika, kwahiyo unapotaka kuondoa na kujenga imani kwa wenye mtazamo mwingine fanya yale yanayotarajiwa ili yaleta imani na kuaminiwa, tumefanya yaliyotarajiwa na sasa yule House Girl hayupo tena, maamuzi ya kitchen party hayapo tena yanakuwa ya maana sasa”
“Kwahiyo Wanawake wasomi na Viongozi wenzangu tambueni kuwa jitihada za kuendelea kuielimisha Jamii yetu kufahamu kwamba usawa wa kijinsia sio mapambano ya Wanawake kutaka kuwa juu ya Wanaume hapana, bali ni hitajio la Ibara ya 12 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania isemayo Binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa, kinachotutofutisha mbele ni malezi na makuzi”
Akitoka huyo apewe zuchuSamia anafaa kuwa Rais hadi 2040,akitoka tumpe Abdul, watatuvusha mbali sana sana.
Akitoka huyo apewe zuchu
Hapana,tunakupendekeza wewe sisi watu wa syteam uchwara!!Akitoka huyo apewe zuchu