Ndugu zangu Watanzania,
Uwanja wa Benjamini Mkapa uliofurika na kumiminika wanachama na mashabiki wa Simba umejikuta ukiripuka kwa shangwe ,nderemo na vifijo baada ya kusikia Sauti ya Mama yetu Mpendwa kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,ambaye amepiga simu kwa katibu Mkuu wa wizara ya sanaa na utamaduni Mheshimiwa Msigwa.
Ikumbukwe Mheshimiwa Rais yupo ziarani mkoani Morogoro na kutumia muda huu wa mapumziko ya jioni kufuatilia Siku hii ya Wenye Nchi yaani Simba Day.
Kwa hakika Rais Samia anapendwa haijapata kutokea hapa nchini.hakuna kama Samia na hakuna mwenye kumfikia katika ushawishi na kupendwa na watanzania.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
View attachment 3060866
Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.