Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika mkutano wa nchi zenye uchumi mkubwa duniani G20 alipata nafasi ya kueleza mikakati ya Tanzania ya kujitosheleza kwa chakula na kulisha nchi zingine Afrika.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano huo wa G20 kuhusu mambo yaliyojadiliwa katika mkutano Rio De janeiro Brazil siku ya Jumatatu na Jumanne.
Alisema kama Tanzania haitakumbwa na madhara makubwa ya mabadiliko ya tabia nchi basi itakuwa na uwezo wa kujitosheleza kwa chakula chake na kulisha majirani.
Alisema pamoja na hayo bado kuna maeneo ambayo iwapo yataongezewa nguvu hali ya uzalishaji wa chakula itakuwa bora zaidi na kutaja mambo hayo kuwa ni tafiti mbalimbali, matumizi ya mashine na mbolea.