Wengine ambao wameibiwa mifugo na hawatapata nafasi maisha yao yote kukutana na Rais tatizo lao litatatuliwaje??Umejuaje kama huyo mwananchi alitaka kuuliza swali binafsi, haya tuchukulie suala binafsi labda mwananchi kaibiwa mifugo yake...Rais si anampasia DC kulishughulikia, inakuwa ni agizo sasa la Rais kwasabb hawa viongozi wetu huku mawilayani saa zingine wanapenda sana ubwanyenye wanachelewa kuchukua hatua!.
Dubai na OmanYeye ni Rais wa nchi gani?
Angemusikiliza tu pia angejua sehemu gani muhusika anatakiwa kutatua hilo tatizo, DED, RC , DC etcRais Samia leo September akiwa mkoani Mtwara alisimamisha msafara wake kuongea na wananchi wa eneo hilo. Moja wananchi hao aliomba kuongea jambo ambapo Rais alimwambia mambo ni mengi na Tanzania ni kubwa.
Rais Samia alimtaka mwananchi huyo ampatie jambo lake mbunge kisha amfikishie Rais au wasaidizi wake.
Mwaka 2017 Rais Magufuli akiwa anaelekea Mtwara alisimamishwa Somanga na mwananchi aliyeelezea changamoto ya zahanati katika eneo hilo kutokamilika kwa miaka mingi. Rais Magufuli alichangia na kuamrisha ikamilike.
Alipopita tena barabara hiyo miaka 3 baadae mwananchi huyo alimzawadia jogoo kama shukrani ya kutimiza ahadi ya kufanyia kazi dukuduku lake na Magufuli alimsubiri mpaka alipomkamatia na kumpa. Alipofariki, mwananchi huyo alifunga safari kumzika Rais Magufuli mwaka 2021.
Huyo mmoja sindio atawakilisha wengine wote wenye matatizo yanayofanana, huelewi nn sasa hapo.Wengine ambao wameibiwa mifugo na hawatapata nafasi maisha yao yote kukutana na Rais tatizo lao litatatuliwaje??
Sahihi kabisa, utaratibu wa Rais kusikiliza shida za mtu mmoja mmoja barabarani haufai
Hiv we unajua thamani uipatayo mtu akikusikiliza, Je si thamani kubwa zaidi kama utasikilkzwa na raisi? Acha kushabikia ujinga, yeye ni Raisi hata kama asingempa jibu pale, anagemuhakikishia kuwa watu wake watalifuatilia, ingeleta maana. Kusikiliza wananchi ni kuwaheshimu. Sasa ngoja 2025 ije tuone kama hatojibu mtu.... Uongozi ni kipaji bana... Hili si lake ni tu kubali ndio Maana kakosa hekima ya namna ya kulihandle.Haya mambo tumeyaona awamu ya tano, hakukuwa na lolote la maana
Dawa ni kuimarisha mifumo iliyopo tu la sivyo itakuwa kutwanga maji kwenye kinu na kutafuta sifa za bei rahisi
Hapo alisema naagiza ma RC wote nchi kusghulikia matatizo yote yanayofanana na la Mwananchi huyu mara Moja na masuala mengine ambayo ni kero kwa Wananchi. Mchezo ungisha kiukaini!Wengine ambao wameibiwa mifugo na hawatapata nafasi maisha yao yote kukutana na Rais tatizo lao litatatuliwaje??
Na wakati wa kuomba kura basi amtume huyohuyo Mbunge tusimuone huku kwetu maana inaonekana shida zetu hazimuhusu yeye. Sijui tumepata Rais wa aina gani huyu ambaye hataki hata kufahamu changamoto za raia wake. It's very hectic kwa kweli
Rais wa MatajiriYeye ni Rais wa nchi gani?
Mmmh🤣🤣🤣🤣🤣Wasimsumbue rais wetu, kwanza hawakumchagua🤣🤣🤣