Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Umejuaje kama huyo mwananchi alitaka kuuliza swali binafsi, haya tuchukulie suala binafsi labda mwananchi kaibiwa mifugo yake...Rais si anampasia DC kulishughulikia, inakuwa ni agizo sasa la Rais kwasabb hawa viongozi wetu huku mawilayani saa zingine wanapenda sana ubwanyenye wanachelewa kuchukua hatua!.
Wengine ambao wameibiwa mifugo na hawatapata nafasi maisha yao yote kukutana na Rais tatizo lao litatatuliwaje??
 
Sasa kama hataki kusikiliza wananchi ambao yeye mwenyewe kawafuata ili azungumze nao, anakwenda huko kufanya nini sasa?

Si Angelala tu huko ofisini kwake ili hiyo kazi wafanye hao wabunge au ma DC au ma RC na watendaji wa vijiji na wao wampelekee ripoti tu?

Huyu mama bila shaka ana shida fulani upstairs na kutojua mamlaka na madaraka ya maamuzi aliyonayo au pengine tayari amesharogwa na kulewa cheo cha Urais na kumpa kiburi na dharau.!!
 
Rais Samia leo September akiwa mkoani Mtwara alisimamisha msafara wake kuongea na wananchi wa eneo hilo. Moja wananchi hao aliomba kuongea jambo ambapo Rais alimwambia mambo ni mengi na Tanzania ni kubwa.

Rais Samia alimtaka mwananchi huyo ampatie jambo lake mbunge kisha amfikishie Rais au wasaidizi wake.

Mwaka 2017 Rais Magufuli akiwa anaelekea Mtwara alisimamishwa Somanga na mwananchi aliyeelezea changamoto ya zahanati katika eneo hilo kutokamilika kwa miaka mingi. Rais Magufuli alichangia na kuamrisha ikamilike.

Alipopita tena barabara hiyo miaka 3 baadae mwananchi huyo alimzawadia jogoo kama shukrani ya kutimiza ahadi ya kufanyia kazi dukuduku lake na Magufuli alimsubiri mpaka alipomkamatia na kumpa. Alipofariki, mwananchi huyo alifunga safari kumzika Rais Magufuli mwaka 2021.

Angemusikiliza tu pia angejua sehemu gani muhusika anatakiwa kutatua hilo tatizo, DED, RC , DC etc
 
Wengine ambao wameibiwa mifugo na hawatapata nafasi maisha yao yote kukutana na Rais tatizo lao litatatuliwaje??
Huyo mmoja sindio atawakilisha wengine wote wenye matatizo yanayofanana, huelewi nn sasa hapo.
Tena kupitia huyo mwananchi mmoja Rais anaweza akatumia nafasi hiyo kuwapa maagizo ma DC's wengine kote nchini namna ya kushughulikia kero za aina hiyo.
 
Sampling hufanyika popote ilmradi inaweza saidia pata matokeo, binadam wa leo wamejiwekea limitations hata ktk kufikilia wakidhani kuwaza tofauti ni uchochezi
Sahihi kabisa, utaratibu wa Rais kusikiliza shida za mtu mmoja mmoja barabarani haufai
 
Haya mambo tumeyaona awamu ya tano, hakukuwa na lolote la maana
Dawa ni kuimarisha mifumo iliyopo tu la sivyo itakuwa kutwanga maji kwenye kinu na kutafuta sifa za bei rahisi
Hiv we unajua thamani uipatayo mtu akikusikiliza, Je si thamani kubwa zaidi kama utasikilkzwa na raisi? Acha kushabikia ujinga, yeye ni Raisi hata kama asingempa jibu pale, anagemuhakikishia kuwa watu wake watalifuatilia, ingeleta maana. Kusikiliza wananchi ni kuwaheshimu. Sasa ngoja 2025 ije tuone kama hatojibu mtu.... Uongozi ni kipaji bana... Hili si lake ni tu kubali ndio Maana kakosa hekima ya namna ya kulihandle.
 
Wengine ambao wameibiwa mifugo na hawatapata nafasi maisha yao yote kukutana na Rais tatizo lao litatatuliwaje??
Hapo alisema naagiza ma RC wote nchi kusghulikia matatizo yote yanayofanana na la Mwananchi huyu mara Moja na masuala mengine ambayo ni kero kwa Wananchi. Mchezo ungisha kiukaini!
 
Hao wananchi nao ni wajinga tu,wangeacha kupoteza muda wao huko barabarani wasubiri wabunge wao tu.
 
Ukiwa kiongozi lazima uwe very humble, Lazima ujishushe sana hata kama ni kwa unafiki, Alichokifanya huyu Mama ni Ujinga mkubwa sana, No mfano mbaya sana kwa viongozi wengine wa serikali.
 
Na wakati wa kuomba kura basi amtume huyohuyo Mbunge tusimuone huku kwetu maana inaonekana shida zetu hazimuhusu yeye. Sijui tumepata Rais wa aina gani huyu ambaye hataki hata kufahamu changamoto za raia wake. It's very hectic kwa kweli

Washauri wake wako wapi? Au hawajali? Ali mradi wao wanaingiza hela zao mfukoni, akiharibu atajijua yeye mwenyewe. Hii ni aibu kwa hicho kiti.
 
Amekataa kuingia kwenye mtego wa kupigwa pesa kizembezembe kama yule Bwana aliyegeuzwa na waungwana kuwa fursa ya kujipatia kipoto.
 
Inawezekana huyo mbunge ndio tatizo au tatizo analijua na halisemei,au mbunge haonekani/ hapatikani/hafiki maeneo hayo.Kama aliamua kusalimia wananchi kusikiliza sample mbili tatu za wananchi sioni tatizo.Labda yalimcheza ataulizwa kuhusu bandari!
 
Back
Top Bottom