GE2025 Rais Samia akiapishwa Urais aongoze nchi bila kuwabembeleza Watanzania wala kuwapa Uhuru Uliopitiliza

GE2025 Rais Samia akiapishwa Urais aongoze nchi bila kuwabembeleza Watanzania wala kuwapa Uhuru Uliopitiliza

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ndugu zangu Watanzania,

Sisi watanzania ni watu wa ajabu sana ,ni watu wa kushangaza sana ,ni watu ambao tupo tofauti sana na watu wengine. Watanzania ni watu ambao ukiwapa uhuru wa jambo fulani unakuwa umeharibu kabisa. Kwa sababu watatumia uhuru huo na kukuchukulia wewe uliyewapa uhuru huo kama Mjinga na usiyejitambua.

Watafanya kila aina ya vituko na uharibifu, wataingiza kila aina ya hasara na kuleta kila aina ya uharibifu . Leo hata jaribu uwe na kampuni yako au biashara yako kubwa kubwa na mtaji wa mamilioni halafu umkabidhi mtanzania na kumpatia uhuru mkubwa pasipo kumfuatilia kwa ukaribu . Ukirudi baada ya mwezi mmoja kuja kupiga hesabu na kuangalia maendeleo ya biashara yako au kampuni yako utakachokikuta kitakububujisha machozi ya huzuni.

Kwa sababu utakuta mtaji haupo ,faida hakuna ,vitu havipo na hata jengo limeharibika kabisa. Kwa sababu mtanzania ukimpa uhuru unakuwa umempa mwanya wa kuiba ,kuharibu na kutapanya hovyo hovyo.utakuta amebeba kila kitu na kuficha sehemu .

Embu fikiria hawa watanzania ambao wakati wa Awamu ya Tano walilia na kupiga mayowe na Makelele kuwa Rais Magufuli alikuwa ni Dikteta na aliyeendesha Nchi kidikteta. Na wakaenda mbali zaidi wakawa wanamkumbuka sana Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt Jakaya Kikwete na kumpongeza kwa kuimarisha Demokrasia na uhuru wakati wa uongozi wake.

Alipoingia Madarakani Rais wetu Mpendwa akawapa watanzania kile walikuwa wanahitaji . Kwa kutoa uhuru wa kutosha kwa watu,kufungulia vyombo vya habari na magazeti yaliyokuwa yamefungiwa na kunyang'anywa Lesseni zao,kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa na mengine mengi sana kama vile kufuta kesi zote zenye sura ya kisiasa ,kukaa mezani na wadau mbalimbali wa siasa na viongozi wa vyama vya siasa na kufanya maridhiano ya mambo mbalimbali.

Lakini cha Ajabu wale wale waliopewa uhuru na yote waliyokuwa wakiyahitaji wakaanza kumtukana Mama yetu kwa matusi ya kila aina ya nguoni ya kuandika na yasiyo andikika. Vitoto vidogo vilivyokosa adabu na malezi mazuri kama vya akina Mdude vikaanza kumtusi na kutumia lugha chafu za kumdhalilisha Rais wetu.

Watu kama akina Lissu ambao walikuwa wamekimbia Nchi wakati wa utawala wa Awamu ya Tano wakaanza kumdhalilisha Rais wetu,kutumia lugha za ubaguzi kwa Rais wetu na kila aina ya maneno ya uongo,uzushi ,chuki na kumchafua Rais wetu kwa chuki tu binafsi . Jambo ambalo lilikuwa na kimekuwa likiniumiza sana Moyo Wangu na kunipa hasira sana kuona Mama yangu na Rais wetu akitukanwa na kudhalilishwa mitandaoni na hata majukwaani.

Mpaka nikajiuliza huu ndio uhuru ambao hawa watu waliutaka ? Haya ndio mambo waliyoyataka kuyafanya wakipewa Uhuru? Niliumia sana kuona watoto wadogo ambao wengine ni wadogo kwa watoto wa Mama yetu Mpendwa wakibetua midomo yao na kumtusi Rais wetu. lakini hao hao watanzania waliokuwa wakimsifia pia Mstaafu wetu Mheshimiwa Daktari Jakaya Kikwete. Leo wamegeuka na wanaanza kumporomoshea Matusi huko mitandaoni na hadi kufikia hatua ya kumuombea Hata Kifo. Hivi huu siyo ushetani kweli? Siyo uchawi huu kweli?

Ndio Maana nasema sasa yatosha ,sasa ni Mwisho ,Sasa kubembelezana na Kuwabembeleza Watanzania iwe Mwisho pale Rais Samia atakapo apishwa kuwa Rais wetu kwa Awamu ya pili. Ikawe hakuna kucheka na mtu wala kumbembeleza mtu atakaye kwenda kinyume na katiba ,sheria , miongozo,taratibu na kanuni. Mtu akifanya hovyo ni kutupa ndani huko akili ikamkae sawa huko.

Mtu yupo hapa hapa Nchini na ametukana na kumtukana Rais wetu na kumdhalilisha Rais wetu . Haraka sana askari wetu tafuta mtu huyo popote alipo na kwa gharama yoyote ile tupa ndani ya gari na kwenda naye kituoni kufanya naye mahojiano na kisha kumpeleka mahakamani.

Ni Lazima Rais wetu aheshimiwe na watu wote na siyo kuchezewa au kudhalilishwa kijinga jinga. Kila mmoja ni lazima ajue Rais na Mkuu wa Nchi siyo sawa na Rais wa Bao au Rais wa Club ya Mpira au Rais wa Bendi ya Mziki .kila mmoja ni lazima ajue ya kuwa RAIS wa Nchi ndio Nembo yetu na Alama ya heshima kama Taifa inayopaswa kuheshimiwa.

Hii ya kubembelezana ndio Sababu watu kama akina Askofu Gwajima wanatoka hadharani kwa kiburi na jeuri bila hofu wala adabu wala staha na kuanza kutoa Maneno ya vitisho na kuipa Amri serikali na kila aina ya Uzushi ,uongo na uchonganishi wa kutaka serikali na Rais wetu achukiwe . halafu mtu huyo huyo anatamka kwa kiburi na jeuri kubwa sitoki ndani ya chama na nitabakia humu humu.

Hii haiwezekani hata kidogo. Ni lazima adabu na heshima iwepo na kutawala. Ifike wakati mtu ajiulize mara mbili mbili kabla ya kutoka hadharani na kutamka jambo au maneno yake. Narudia tena kusema kuwa mtanzania hapaswi kubembelezwa au kupewa uhuru Uliopitiliza. Ni lazima awekewe mipaka na kucholewa mstari ambao kila mmoja ajue ya kuwa hapaswi kuuvuka na kwamba akiuvuka atawajibishwa kwa mujibu wa sheria na katiba.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Huyu ndo MBWA sasa...!!

CC kina kirefu, Moise Aimar, fazili, Mwande na Mndewa, Technologiest, comrade_kipepe, Izato, Lucas mwashamba, Zee la choji,
 
Back
Top Bottom