Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Siku ya leo Januari 8, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua Skuli ya Sekondari Misufini, Bumbwini Zanzibar tarehe 08 Januari, 2025 wakati wa shamrashamra za kuelekea miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika hotuba yake Rais Samia aligusia yafuatayo:
Katika hotuba yake Rais Samia aligusia yafuatayo:
- Aliomba watendaji wa kiserikali na watumishi wa shule hiyo wafanye kazi kwa uadilifu ikiwemo kutunza na kulinda mali za shule hiyo mpya ili iweze kudumu kwa muda mrefu na isipate uchakavu ndani ya muda mfupi
- Aliwakumbusha wananchi kuhusu dhana ya mapinduzi visiwani Zanzibar akidokeza kuwa kwa sasa Zanzibar inajikita zaidi katika maendeleo na mapinduzi ya kiuchumi mara baada ya kupata uhuru wake wa kisiasa mwaka 1963.
- Ameomba shule hiyo mpya iitwe Balozi Seif Sekondari kwa ajili ya kumuheshimisha makamu wa Urais wa pili kutoka Zanzibar Balozi Seif.